Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 348
Kutokana matatizo ya ndoa yanayoikabili jamii kuzidi kuongezeka, nivizuri wanawake nao wakajitosa kuanza kuwa washenga. Mara nyingi ukimpata mwanamme mshenga, huwa haangalii mambo mengi kama tabia ya mchumba wako na kukupa ushauri unaohitajika ili uweze kufanya maamuzi hata kama ni dakika ya mwisho. Kwa vile wanawake wanafahamiana vilemba, wanaweza sana kusaidia katika kuimarisha ndoa ili ziweze kudumu. Mke anaweza kuwa muwazi zaidi kwa mwanamke mwenzake pale ambapo analalamikiwa na mme wake kuliko mwanamme akiyapeleka malalamiko hayo kwa mshenga mwanamme mwenzake. Hii inawanyima wanawake wengi fursa ya kujieleza; Mfano, kama mwanamme hana utalaam wa kumridhisha mke wake!
Nakumbuka kuna wakati wanawake waliomba pendekezo hili ili waweze kufanya kazi za ushenga lakini wanaume wamekuwa wagumu sana kuitikia na kupokea wazo hili. nadhani huu ni wakati muafaka kwa wanawake kudai haki hii ambayo imekaliwa na wanaume ikiwakandamiza na kuwanyima wanawake fursa mbalimbali.
Nawasilisha.