Wanawake: Ni kweli ni wajibu wangu kukutunza na kukuhudumia lakini hata asante hakuna?

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Habari za humu ndani,

Baada ya kusherehekea sikukuu ya wanawake duniani ambayo kwa upande wangu sijaona wanawake wenyewe wakishiriki kikamilifu.

Sasa tuendelee na harakati za maisha kama kawa. Mwenzenu kuna jambo linanitatiza au pengine mimi napenda kupewa sifa sana mnishauri niepuke hili kama nimepitiliza.

Au kwa sababu pesa zenyewe nazipata kwa kuunga unga sana, jasho na mchoko wa kufa mtu na wakati mwingine kashifa, fedheha na matusi huyapata katika harakati za kutafuta kipato.

Mara nyinga si mara zote huyu mwenzi wangu hata nimfanyie nini, pesa si nyingi nazompa lakini najitahidi kadiri ya uwezo wangu lakini kwake neno asante baba fulani, au asante kwake ni jambo gumu kwake.

Sasa naanza kukata tamaa kwamba mwenzangu hana shukurani, au mimi ndio napenda sana kushukuriwa.

Je nifanye nini? Au ni tende wema na kwenda zangu? Je kuna wanawake wa aina hii na si kwangu tu.

Waswahili wanasema asante ni kuomba tena, mtu kwangu akiniambia asante nafarijika sana najisikia raha moyoni, naona kile nilichofanya kimeleta impact kwa mtu huyo hata kama asante yake haitoki moyoni mimi sijali.

Karibuni kwa mjadala maoni na michango yenu.
 
Kushukuru ni tabia ya mtu. Mwingine anahisi akikushukuru utamuona ana uhitaji sana. Kama unampenda tenda wema wende zako mkuu. Ni ngumu kumfundisha mtu mzima baadhi ya tabia ukubwani. Anaweza akawa anafurahia unachompa ila hajawahi kujifunza kutoa shukrani inapobidi ndo sababu anashindwa kusema asante.
 
Iliandikwa kwa jasho lako utaishi....
Yeye kwa uchungu atazaa...

Kuna vitu vidogo sana utakua uvifanyi ambavyo haviusiani na ela...
Wanawake ni viumbe vya ajabu sana... utawapa kila kitu ila mda wako akiukosa nia tatizo.
 
Neno "ahsante" ni dogo lakini lina maana kubwa sanaa,.kuna watu wako hivyo hawana shukrani hawajui kushukuru,wao hudhani shukrani au kusema ahsante mpaka ujengewe ghorofa au ununuliwe Bugatti,. Ukijua kushukuru kwa kidogo huwezi kushindwa kushukuru kwa kikubwa,.mkuu unapaswa kumwambia usimlazie damu huyo hiyo tabia yake ni mbaya na inakatisha tamaa,.mkanye la sivyo ataishia kwenye mambo madogo madogo tuu, makubwa atayasikia redio.
 
huyo ndo alivyolelewa hvyo,inapaswa akushukuru embu jarbu kumnyima uone reaction yake au mweleze ukwel
 
Mara nyinga si mara zote huyu mwenzi wangu hata nimfanyie nini, pesa si nyingi nazompa lakini najitahidi kadiri ya uwezo wangu lakini kwake neno Asante Baba fulani, au asante kwa.....ni jambo gumu kwake. Hili ni gumu sana kwa baadhi, wapo wanawake wapo smart sana kushukuru.....!
 
Km mie mkuu usipokaa sawa naweza shukuru hadi machozi,

Hili jambo limempa mwenzangu ari ya kutupenda na kututunza sana kwa gharama zote!!
 
Pole sana mkuu yaan mm kusema asante kwa mwanaume wangu ni jambo rahisi sana yaan hadi yy mwenyewe huwa anashangaa, hata akinitumia vocha ya buku tu mm nashukuru balaaa na majina ya mahaba nikimuita
 
Kushukuru ni tabia ya mtu. Mwingine anahisi akikushukuru utamuona ana uhitaji sana. Kama unampenda tenda wema wende zako mkuu. Ni ngumu kumfundisha mtu mzima baadhi ya tabia ukubwani. Anaweza akawa anafurahia unachompa ila hajawahi kujifunza kutoa shukrani inapobidi ndo sababu anashindwa kusema asante.
Watu wa hivi Mara nyingi ni wabinafsi sana na wachoyo..chako chake,chake chake...
 
Mfundishe mkuu kusema asante na umuelekeze umuhimu wa kusema asante pia wewe unasemaga asante akikuwekea maji ya kuoga,akikupikia chakula???
 
Kushukuru ni tabia ya mtu. Mwingine anahisi akikushukuru utamuona ana uhitaji sana. Kama unampenda tenda wema wende zako mkuu. Ni ngumu kumfundisha mtu mzima baadhi ya tabia ukubwani. Anaweza akawa anafurahia unachompa ila hajawahi kujifunza kutoa shukrani inapobidi ndo sababu anashindwa kusema asante.
Lakini inauma
 
unabusara sana kipenzi changu ndo raha ya kupata mtoto aliyefundwa
 
Back
Top Bottom