Wanawake ndio wapiga kura wengi wa CCM wanawanyima elimu ili wawatawale vizuri nao wanashangilia

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,568
2,000
Habari wadau!

Nimekaa nimetafakari maamuzi ya serikali hii inayojinasibu ya wanyonge sijui wanyonge hao ni kina nani?

Navyojua wanyonge ni wale wasio na sehemu ya kusemea ndio maana kukawa na makundi maalum kama ya wanawake na watoto wa kike.

Sasa hili kundi la watoto wa kike linakumbana na madhira mbalimbali ikiwemo mimba na ndoa za utotoni ikiwa inamaana mtoto akiolewa bila kutaka ndo mwisho wa elimu kwake au akipewa ujauzito nayo ndio mwisho wa elimu kwake.

Sasa kuwa na wizara ya wakina mama na watoto naona haina haja ifutwe tu sasa kama tunasema mtoto hajitambui na bado tunamuhukumu nini maana yake?

Unampa kwa mkono wa kulia unamnyang'anya kwa mkono wa kushoto ndo serikali hii.

Sasa ccm inatumia silaha hii kuwapata wapiga kura wajinga ili itawale vizuri na tena nashangaa wanawake wa ccm wakishangilia wakati huo wanadai upinzani hawawapendi wanawake hivi ni kweli,? Hawa wamama wetu wa baadae tunawaandaliaje maisha ya baadae na kauli za kusema kuwa ukimwelimisha mwanamke umeelimisha taifa?

Sasa inamaana tunaenda kulifanya taifa la wajinga?
 
Mama Obama

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
1,569

'
Haswa taifa la wajinga. Wanawake tumekuwa wajinga, watoto wetu wakiolewa na miaka 13 tunashangilia. Wakiamuliwa kufukuzwa shule tunashangilia. Watu kama Mama Kikwete waliopata nafasi ya kuingia Ikulu ndiyo wangewatetea hawa watoto, lakini ndiyo anapigilia musumali ati dini zote zinakataza. Kuna maovu zaidi ya ufisadi, kujirundikia Mali za wengi na kuwaadhibu watoto? . Ama kweli wanawake tumekuwa kama ng'ombe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom