Wanawake nchini Rwanda kujilipia mahari ili waolewe

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,738
2,279
Katika kijiji cha Nyamashekhe kilochopo mkoa wa magharibi nchini Rwanda kumekithiri utamaduni wa wanawake kulipa pesa kwa mwanaume ili waolewe.

Mtindo huo mpya wa maisha umezua gumzo katika jamii huku baadhi ya watu wakihoji hatima ya siku zijazo za utamaduni wa kulipa mahari.

BBC imetembelea kijiji hicho na kuzungumza na wanawake, wanaume, viongozi wa kijiji na baadhi ya wahusika ili kufahamu zaidi kwa nini utamaduni huo unazidi kupata umaarufu

Kaitesi Lilian mmoja wa kina mama wa kijiji hicho anasema "Mvulana anapokuja kumposa msichana wako unajua kwamba mambo yameiva, lakini ndoa ikikaribia unaskia kwamba amemgeuka na kumwambia kwamba ndoa haitawezekana ikiwa hatapewa pesa za mahari".

Alipoulizawa mbona wanawake wengine wameolewa bila kufuata utaratibu huo alifafanua kwa kusema"Wakati huo binti alikuja na kuangua kilio huku akinishinikiza niuze kila kitu hata mabati au shamba ilimradi yeye apate pesa ya kumpa mchumba wake.

Tofauti na maeneo mengine ya nchi ambapo mwanaume ndio hutoa posa kwa familia ya mwanamke, utamaduni huu mpya unawashinikiza wasichana kumlipa pesa mwanamume.

Inasadikiwa kuwa pesa hizo ni kama dola 1500(milioni 3... za Tanzania)na huongezeka kulingana na uwezo wa familia ya msichana.

Waliyoshuhudia wanasema pesa hizo lazima zipatikane kwa udi na uvumba.

Lakini ni nini kinacho wafanya vijana kugeuza utamaduni uliopo?

Katika tamaduni za wanyarwanda mahari lazima itolewe tena na bwana harusi mtarajiwa.

Hata kama mahari haijakamilika kwa wakati huo familia husika zinakubaliana jinsi itakavylipwa, na hatimae harusi hufanyika

Katika mkoa wa msgharibu nchini Rwanda pesa hizo zikikosekana hakuna harusi tena.

Kaibanda Bernard ameiambia BBC kuwa vijana "Wanafanya hivyo wakisema idadi ya wasichana sasa hivi ni kubwa sana''

Wasichana wengine wameshindwa kuvumilia, ambapo msichana akitinga umri wa miaka kumi na tano hivi anatafuta pesa kwa nguvu ili aweze kumnunua bwana.

Vijana wenyewe wanaona ni ishara ya ushirikiano katika familia mpya kutokana na hali ya maisha ilivyo ghali siku hizi. John Gatera anasema mmoja wa watu wanaounga mkono mtindo huo wa maisha anasema "Zamani kutoa mahari ilikuwa ni kitu rahisi sana ni ngombe labda na kiwanja lakini sasa hata kupalilia sehemu ya ujenzi lazima ulipe pesa''.

Anasema yeye binafsi akifikisha umri wa kuoa lazima msichana amlipe pesa la sivyo harusi haitafanyika.

Baadhi ya watu katika kijiji cha Nyamashekhe wanataka serikali kuingilia kati suala hilo.

Mmoja wao ni mzee Kaihura ambaye anasema''Kijana hawezi kupata heshima katika jamii ikiwa hatatoa mahari''.

Utamaduni huu mpya umepokelewaje?
Wazazi waliyo na mabinti waliyofikisha umri wa kuolewa wana wasiwasi huenda mtido huo mpya wa maisha ukaenea kote nchini ikiwa hatua hazitachukuliwa kuukomesha. Pia wanahofia suala hili huenda likabadilisha kabisha utamaduni wa jadi wa wanaume kulipa mahari.

Vijana hususana katika mkoa huo wanadaiwa kujiona ''mastaa'' hali ambayo huenda ikawafanya kuzembea majukumu yao ya familia hata wakifanikiwa kupata mwake zao. Sio mara ya kwanza Mkoa huo wa Magharibi ambao ndio mkubwa kuliko mikoa mingine kuzua gumzo kuhusiana na masuala ya kijamii.

Kabla ya mtinduu huu wa sasa wa vijana kutaka walipwe pesa na wasichana ili wawaoe, kulikuwa na wakati inadaiwa kuwa mvulana akimtembelea mchumba wake kwao sharti achinjiwe kuku.

Chanzo BBC
 
Poa , ili kukomesha mahari hasa wale wanaotoa ng' ombe wengi , akishapata ujauzito wakati wa uchumba mwambie kila mtu akae kwake ila tulee mtoto pamoja . Ukiulizwa kulikoni sema huna mahari .
 
ntashangaa kama bado upo Tanzania wakat ushaiona fursa
 
nyakati zile zilizotabiriwa kwente bible zabisha hodi, itafika kipindi wanawake watatu wanataka bwana mmoja kwa pamoja ili wasitiriwe na aibu
Ni Saba Mkuu sio Watatu, isaya 4, 1-2.. Binafsi nasubiria sana Kipindi Hiki Kifike!
 
Back
Top Bottom