Wanawake naomba mnijibu hili juu ya utafutaji na discipline ya Fedha

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,962
Kuna kasumba miongoni mwa wanawake kuwa wanapoingia kwenye mahusiano na mwanaume kuanzia hatua za awali na hata ndani ya ndoa, basi ni mwanaume pekee ndie anawajibika na gharama za maisha na si mwanamke.

Na hata wanawake wenye ajira kwa maana ya kazi awali ya mahusiano wanapoingia katika mahusiano ghafla wanahamishia mzigo wa gharama zao za maisha kwa mwanaume atakaye kuwa nae kwa wakati huo.

Najiuliza sasa, hii imekaaje aiseee? Kwanini wanawake mkiwa wenyewe mnatumia akili zile za maisha ambazo hata mama zetu walikuwa nazo miaka hiyo tena ndani ya ndoa na ndio maana wakajiheshimisha kwa wazee wetu na wakawa wajenzi wazuri wa familia.

Changamoto ninyi kazazi cha sasa, unakuta mwanamke umemkuta amepanga chumba kimoja au chumba sebule, anaishi kwa kujitafutia mwenyewe, ukiingia katika mahusiano nae na kutaka aje kuishi na wewe na kujenga mazingira ya kuchumbiana anaanza Drama za kitoto, kukutegea kwa kila kitu, hashiriki katika jitihada za utafutaji yaani ni as if anataka akusabotage ufeli Maisha kisha yeye aondoke arejee katika maisha yake.

Yaani tasks simple tu kama kupanga na kusimamia budget za nyumbani atajifanya kuwa ni kazi sana kwake kuzifanya, kusimamia ada za watoto, yaani zile vitu ambazo akiwa mwenyewe huwa anafanya bila shida akishaanza mahusiano na mwanaume anamtwisha vyote na anaanza kujifanya ni kiazi kwenye maisha hakuna analolijua. Anakuwa busy zaidi na uharibifu na vituko kama kufumania sms za michepuko, kulalamikia issue za kipuuzi kama mwanaume kuchelewa kurudi home, na vitu visivyo na mbele wala nyuma.

Wanawake hili swali nijibiwe, ni kwamba mnamalengo ya kuifelisha hii jamii ya mtanzania, mnataka kumsaidia shetani kazi ya kuporomosha familia na kumjengea jeshi lake la hovyo, au mna ajenda gani?
 
Me Naona inategemeana na mtu tu..kuna wanawake wanafanya kazi mshahara ukitoka anamuuliza mumewe wafanyie nini pesa yake
 
Back
Top Bottom