bongompya
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 224
- 43
Safu hii inaendelea kuwaletea elimu kubwa ili kuwaweka wasomaji wake kwenye uelewa mkubwa kuhusu mapenzi na maisha.
INAVYOJULIKANA
Mara nyingi wanaume wamekuwa wakitajwa kama sababu kubwa ya wanawake kutofikakatika matarajio ya safari ya tendo la ndoa pindi wanaposhiriki.Hii inatokana na ukweli wa kibaiolojia kuwa, mwanaume wa kawaida hufika mwisho ndani ya wastani wa dakika 2.3 hadi 5 wakati mwanamke hufika kwa wastani wa dakika 15 hadi 20.
TABIA ZA WOTE
Ukiachilia mbali utofauti huo wa dakika, pia mwanaume wa kawaida mara baada ya kufikia mwisho hutumia dakika 15 hadi 30 ili aweze kurudia tena lakini kwa mwanamke huwa tofauti kwani huweza kuendelea zaidi bila kuwa na muda huo wa mapumziko.
Hivyo basi kwa tafsiri ya kawaida, mwanaume ana kawaida ya kuwahi kufika mwisho huku mwingine akiweza kurudia hadi pale mwanamke naye atakapofika.Wanaume wenye matatizo yanayotajwa kama upungufu wa nguvu za kiume wakishindwa kurudia tendo hilo hubeba lawama za kutowaridhisha wapenzi wao au wake zao.
UTAFITI WA KARIBUNI
Hata hivyo, tafiti mbalimbali za hivi karibuni zimebaini kuwa, asilimia 31 tu ya wanaume ndiyo wana matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume huku wanawake wao, asilimia 43 wakitajwa kuwa na matatizo yanayowasababishia kutofika mwisho kitaalamu female sexual dysfunction ‘FSD’ ambayo hata mwanaume awe rijali kiasi gani hushindwa kumfikisha mwisho mwanamke mwenye matatizo hayo.Mbaya zaidi, wanawake wengi hawana ufahamu wa tatizo hilo kwa kuwa hakuna elimu ya kutosha kwenye jamii, suala linalowafanya watoe lawama kwa wapenzi wao jambo ambalo si sahihi bali wana upungufu wa nguvu zao wenyewe.
SABABU ZA TATIZO
FSD kwa wanawake husababishwa na matatizo mbalimbali kama vile magonjwa ya kisukari, moyo, matatizo ya mishipa ya fahamu, matatizo ya homoni, mapafu, ini, utumiaji wa madawa ya kulevya, utumiaji wa baadhi ya madawa makali bila ushauri wa daktari, ajali na sababu nyinginezo kama vile matatizo ya kisaikolojia.
ATHARI ZAKE
Matokeo ya mwanamke kuwa na ugonjwa huu ni kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi hata kama yupo ndani ya ndoa, kuchukua muda mrefu kupata hisia hizo au kutopata kabisa, kuchelewa kuliko kawaida kufika mwisho au kutofika kabisa. Pia kuchoka, kutosikia ladha ya mapenzi au kuwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.Hivyo basi ni vyema kama mwanamke atakuwa na dalili hizo afike katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu ya kitaalam.
Canzo: Chizika