Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
- Thread starter
- #21
loh afadhali madhara hayakuwa makubwa...........
kama ulivyosema ni utegemezi wa hisia, ila pia kuna uoga wa kujitegemea, baadhi ya wanawake hata wawe na kazi nzuri, mishahara mizuri bado wanaogopa kujitegemea anahisi hatoweza kumudu gharama za maisha peke yake hivyo huwakuta wakivumilia matusi, kuna wanaume wanabaka hadi ndugu za mke lakini mke hachukui hatua, anaogopa mume akimuacha hataweza leo/tunza familia, ingawa unaweza kukuta huyo mumewe hachangii hata sukari....
Nimewahi kuzungumza na baadhi ya wanawake wanaoishi kwenye ndoa ngumu, wengi sababu wanazozitoa, ni kichekesho......
Kuna mmoja alidai kwamba, aliwahi kuonywa na wazazi pamoja na ndugu zake juu ya huyo mumewe kwamba sio mume mzuri, nadhani waligundua kasoro zake mapema, lakini yeye aling'ang'ania hadi akaolewa, ni kweli hata yeye aliziona hizo kasoro, lakini alijipa moyo kwamba huenda atabadilika (wenyewe husema akikua ataacha) lakini alipoolewa na mume yule hali ilizidi kuwa mbaya. Sasa anajiuliza, Je akienda kuwaeleza wazazi na ndugu zake kwamba ndoa imemshinda watamuonaje, anahisi watamshambulia na kumdhihaki
Mwingine naye alinieleza kwamba, alipompata huyo mumewe, alijikweza sana kwa marafiki zake kwa sababu mumewe alikuwa na hali nzuri sana kifedha, alidekezwa sana na alijiweka mbali na rafiki zake akihofia kuporwa mumewe, lakini baada ya kufunga ndoa, alifurahia ndoa yake kwa miaka mitano tu, baada ya hapo hali ilibadilika. Mume amekuwa malaya, amekuwa mlevi, na kila akirudi nyumbani lazima wagombane na kuishia kupigwa.............kwa ujumla ndoa yake imekuwa ni ya vurugu kila siku.
Na yeye anadai hawezi kudai talaka kwa sababu anaogopa kujidhalilisha, Je ndugu na marafiki zake watamuonaje?
Kwa hiyo kama ulivyosema, wapo wanawake wanakubali kufa huku wakiona kwa kuogopa kwamba jamii iliyo wazunguka itawaonaje pale watakapoachana na waume zao...................!
Kwa kweli zipo sababu nyingi sana na nyingine ni za kijinga kabisa.................