Wanawake mtuonee huruma sisi wanamume

Wanawake mtuonee huruma sisi wanamume

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
2,245
Reaction score
2,128
Habari zenu, najua weekend iko poa japo kwa wengine majanga tena makubwa.Naomba kila mwanamume asome na ajifunze kitu kuwa wanawake sio ndugu wala rafiki zako kamwe.

Ni hivi juzi nilipandisha uzi hapa JF kuhusu kumlalamikia jirani yangu ambaye amehamia hivi karibuni. Kuwa tangu kuhamia kwake sipati usingizi usiku kabisa. Uzi wenyewe ni huu
.
Kusema kweli huyu jirani aliyehamia amejipanga vizuri tu kimaisha ikumbukwe ni(ke) jirani.

Mkasa ulikuwa hivi, Jana mida ya jioni niko zangu home napiga workout mara nikasikia hodi mlango mkubwa nikaenda kufungua geti kuna jamaa amekuja na pikapu akanipa tano nikamkaribisha ndani/uwani.Jamaa inaonyesha hayuko sawa kabisa.Akanza kwa kuniuliza Monica yupo( si jina lake halisi) huku amekunja face nikamwambia hayupo katoka.Msubiri kama vipi basi tukawa tunapiga stori mbili tatu kuhusu maisha.

Baada ya saa moja hivi kupita Monica anakuja home na basha wake.Kufika tu Monica akashtuka kumkuta yule jamaa pale home.Basi yule jamaa aliyekuwa anamsubiri Monica akanza matusi na vurugu home pale.Jamaa"Nimekuja kuchukuwa vitu vyangu nilivyokununulia m*#*πa wewe, Jamaa akazama ndani akachukuwa TV flat screen na hometheater akapakia kwenye gari akaondoka.

Sasa leo mida hii jamaa kaja tena ila Monica na basha wake hawapo.Huyu basha wa Monica ni mjeda/mjeshi.Mi nikamkaribisha ndani akaingia ndani tukawa tunapiga stori.Jamaa akanipa mkasa mzima kuhusu huyu manzi/Monica.

Jamaa"Huyu mal*y* tumeanza mbali bro nimemsaidia vitu vingi sana.Mahusiano yetu yana miaka kama 3 hivi alikuwa mchafu tu mi ndo nimempiga msasa hadi anang'aa hivi".

Jamaa, "Nimemuhudumia vitu vingi sana yaani hata juzi nimemtumia kama laki2 na nusu.

Vitu vyote nimenunuwa Mimi kwa pesa yangu(Jiko la gesi,kabati la vyombo,kitanda+ godoro,kabati la vyombo,flat screen na vitu vingine vingi). Jamaa amekuja na gari kuchukuwa vitu vyake. Jamaa amemnunulia kiwanja na ameanza ujenzi kwa ajili ya Monica.Yaani kifupi jamaaa kavurugwa sana.

Jamani tunajitahidi kuwahurumia sana sisi hawa sana wanawake lakini hawana huruma na sisi.Tuwe makini sana wanaume wenzangu
 
Duh! Sasa naye anahudumiaje hivyo wakati hata hajamuoa? Mi namuona fala tu huyo jamaa.

Halafu sijui kwanini asilimia kubwa ya wajeda wanakuwa dhaifu sana katika mapenzi?!
 
Ladies who likes money and cars are called "MONICA" so awe makini na hao viumbe vinavyoitwa MONICA.

Inawezekana mana hata teknoofficial kamwimbia monica

Wanatunyooosha sana akina monica


Yaaan kapigwa msasa kwanza jamaa hana huruma kwann ampige monica msasa je alkua mchafu kiasi gan hadi msasa daaah


Mm ndo nimeeelewa hvo ko usifosi nielewe kama ww☹️

Pole monica
 
Duh! Sasa naye anahudumiaje hivyo wakati hata hajamuoa? Mi namuona fala tu huyo jamaa.

Halafu sijui kwanini asilimia kubwa ya wajeda wanakuwa dhaifu sana katika mapenzi?!
Nashangaa ila si unajuwa ukiwa katika love unakuwa na matumaini mengi.
 
Mwanamke anahitaji vitu viwili kwa wakati mmoja ktk maisha ya urafiki, uchumba na ndoa, PESA na 6×6 ya kutosha, ikiwa utakuwa na kimoja tu kati ya hivi ujue bado hujakidhi vigezo, hawa viumbe tumeumbiwa lakini ni mateso makubwa, Wanaume waliopo ktk uhusiano wa kawaida na waliopo ktk ndoa wote wanalia milio sawa kama Nokia ya tochi.
 
Huu uzi lazma nicomment.....
Ingawa unaweza ingiliana na zingine ila ni kweli tupu.....


Nilitendwa na mwanamke wangu nilompenda sana tukaachana.....

Baada ya muda nikaja kupata mwanamke mwingine ambaye nilimpenda na yeye nahisi pia alinipenda maana alikuwa free sana na mimi, hakuwa na wasiwasi na kunitambulisha hata kwa ndugu zake wa karibu kama mama yake mzazi, mdogo wake, baadhi ya mashemeji e.t.c....niliona nimepata, hapo tuna kama miezi mitatu tu....cha ajabu huyu dada alikuwa na akili sana, alikuwa na simu mbili, moja utaiona free muda wote juu ya meza, kitandani au popote pale anaiweka, anaweza hata kukupa upige cm ukimuuliza kama ana salio na wewe umeishiwa ghafla, hyo nyingine hutakaa uione imetolewa kwenye pochi, haiitagi wala hata haivibrate!!!!

Cha ajabu huyu dada alikuwa na pesa za ajabu na hana kazi maalumu, ila ana pesa za ajabu ajabu tu.....yaani pesa ipo mpaka kuna kipindi nikawa nahisi labda ni Government Agent au Secret Service coz sijawahi mdaka na mawasiliano na wanaume au vipi ila unaona tu ana ela saana na ile simu yake nyingine ndo ikawa inanipa mashaka.....akipata tatizo anapiga simu moja tatizo limeisha....ukidakwa na askari anapiga simu mnaachiwa...sikuwa namuelewa kabisa......


Kumbe nyuma yake kuna kijana mmoja mwenye uwezo sana anaye kwa muda mrefu sana...na huyo kijana ana malengo ya kumuoa...ila mwanamke anamtumia tu.....siku nimekuja gundua nilimkimbia kama ukoma.....


Nasikiaga yule kijana mwenzangu alikuja kumnyang'anya kila kitu mbeleni yule dada.....


Lesson nilopata: wanaume wenzangu msije mkajidanganya kuhusu pesa, kwamba ukiwa na pesa ndo kila kitu....tafuta atayeendana na wewe, mengine unaweza tambua tu....

Ni hayo tu wakuu
 
Unamjengea demu wakati wewe huna makazi hahahahahaha
Nimekumbuka kuna nyimbo inaimba kumnumnulia simu walipoachana kampokonya sijui hii aliimba nani by the way afanye amehonga maana na yeye kapewa papuchi miaka mitatu wamalizane hivo Tu

Note kuna papuchi tamu huwezi wacha watu walie tu
 
Kala Jeremiah ft. Nay wa Mitego_Simu ya Mwisho. .....ulikuwa mchafu nguo mpaka mwili waakoo.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom