Wanawake msilalamike sana

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
WANAWAKE MSILALAMIKE SANA
Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi. La hasha wanaume wengi tunapenda mambo yafuatayo
1. Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao.Mara nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya upendo waliotoa kabla.
2. Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto.Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu. Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote. Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.
3. Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100. Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe.Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao.
Jiamini kisha uwe muaminifu.Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.
4. Wazo la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari kwa hilo.
Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja.
Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.
5. Wanaume huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na wakarimu.
6. Wanaume hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke. Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo, jirekebishe ili umkune mwenzi wako.
7.Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake.
Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Wale walevi hukosa sifa ya u-mwanamke ambayo wanaume huihitaji.
 
mwanaume kama hakupendi kutoka moyoni mwakevutasugua gaga, utamaliza vitabu vya dini, majarida, mizizi ila hawezi kujisikia comfoetable kuwa nawe maishani mwake ukimganda sana atakuoa halafu atachepuka
 
WANAWAKE MSILALAMIKE SANA
Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi. La hasha wanaume wengi tunapenda mambo yafuatayo
1. Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao.Mara nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya upendo waliotoa kabla.
2. Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto.Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu. Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote. Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.
3. Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100. Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe.Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao.
Jiamini kisha uwe muaminifu.Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.
4. Wazo la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari kwa hilo.
Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja.
Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.
5. Wanaume huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na wakarimu.
6. Wanaume hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke. Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo, jirekebishe ili umkune mwenzi wako.
7.Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake.
Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Wale walevi hukosa sifa ya u-mwanamke ambayo wanaume huihitaji.

Da. Aisee we ni Profesa. Mipoint ya kweli kabisa.

Kula milike 100000000.
 
Hao unaowaongelea wana uaminifu asilimia ngapi?
 
Attachments

  • 1451401440054.jpg
    1451401440054.jpg
    18.9 KB · Views: 64
Sawa hatulalamiki tena ila na nyie mjifunze kutugharamia(mtupe hela ya kutosha), mtugegede vizuri, mtujali na mtupe attention baasi maisha raha mustarehe
 
Back
Top Bottom