Annina, wewe na Fixed Point kimsingi mnazungumza kitu kimoja na mimi sikubaliani nanyi. wewe nitakusamehe kwa vile si mwanume na hujawahi kuwa mwanume, mimi kwa uzoefu wangu ni kuwa watu wengi hawaelewi wanapendeana nini. mtu halisi si yule anayeonekana, la hasha mtu halisi ni yule asiyeonekana. hivyo watu wanaoamini kuwa wanapendana ambao mapenzi yao yamebase kwenye muonekano wa mwenzie ndiyo yenye negative relationship na wakati kwani mwili ukizeeka unapunguza mvuto wake.
upande mwingine, watu waliopendana kwa kubase kwenye hobby, tabia, interests experience na mambo mengine kama hayo yasiyoonekana, graph yao ina positive relationship kwani kadiri mtu anavyozeeka ndivyo mambo hayo yasiyoonekana huwa nayo yanaimarika. hivyo wale watu mnaowaona wanapendana sana uzeeni, ni kwa sababu mapenzi yao yalibase kwenye vitu hivyo...
nawasilisha