1. Kwa mfano, mwanaume hajipendi, mwanamke anapojaribu kuikemea tabia hiyo anakuwa anajenga ukuta mkubwa sana kati yao bila yeye kujua. Inashauriwa, badala ya kumwambia moja kwa moja mumewe kwamba aache kutojipenda, inashauriwa ni vyema akamnunulia mumewe nguo na akizivaa amsifie sana kiasi kwamba mwanaume huyo atajiona kuwa kumbe akivaa nguo za kiwango au mtindo fulani anakuwa katika hali ya kuvutia kupita kiasi. Hapo mwanaume naye atajaribu kununua aina hiyo ya nguo. Kwa wanawake ambao waume zao wana tabia ya kutojipenda kimavazi wanaweza kujaribu hata leo ili wapime matokeo ya ujanja huu.
2. Wanawake wanafanya makosa pale wanaposhindwa kushukuru juu ya yale mazuri wanayotendewa na waume zao na badala yake kulalamika kwa yale ambayo hawakutendewa. Utakuta mwanaume anajaribu kufanya hiki na kile kwa sababu ya upendo alio nao kwa mkewe, lakini mwanamke huyo hata mara moja hashukuru au kuonyesha kwamba anathamini juhudi hizo za mumewe. Lakini pale mwanume anaposhindwa kumfanyia hiki au kile iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi mwanamke hukata kama wembe kwa kauli zake za kulaani na kulalamika. Ni lazima wanawake wafahamu kwamba kwa maumbile wanaume hupenda sana kuonekana kuwa wamefanya mazuri au ni mashujaa kwa wake zao.
3. Kuna wanawake hawajui ‘asante' kwa waume zao hawajui kuonyesha kwamba walichofanyiwa hata kama ni kidogo wamefurahi na kukikubali. Wanawake hawa kwa bahati mbaya wakati huo huo huwa hawajui kuacha kulaumu pale wanapoona hawakufanyiwa yale waliyotarajia kufanyiwa na waume zao. Mwanamke anapaswa ajifunze kusema ‘asante' na kuonyesha kwamba ameridhika na alichotendewa na mumewe. Ajifunze pia kuacha kulalamika sana pale ambapo hakutendewa alichopaswa kutendewa.
4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo.
Wanawake huwa wanakosea sana pale wanapoeleza kukerwa hisia zao kwa kuuliza maswali ambayo hayana majibu, maswali ya kupita, ambayo siyo ya moja kwa moja kuhusiana na maudhi….. "unawezaje kufanya hivyo!" Ni vizuri mwanamke akaelezea kilichomkera moja kwa moja kuliko kutumia njia ya kuzunguka ya maswali yasiyo na majibu. "Sijui ndiyo nikueleweje?" Ni miongoni mwa maswali haya yasiyompendeza mwanaume.
Yummy uko sahihi, lakini kumbuka kwamba nilichoeleza sio mkwamba ni formula ambayo mnapaswa nkuifata kama ilivyo, nilichofanya ni kuandika mfano wa namna unavyoweza kucheza na maneno na vitendo kulingana na namna unavyomjua mumeo.............Nilijaribu hii lakini iligonga ukuta vibaya sana,iliishia mimi ndio niwe namnunulia nguo kila kukicha!!!!!
Kweli hili ni kosa,pale unapofanyiwa kitu kizuri inabidi kushukuru hata kama ni kidogo lakini amejaribu. Hakuna kitu kizuri kama kuonyesha kuwa umefurahia mume alichojaribu kukufanyia inasaidia kumpa moyo ili afanye zaidi na baadae kujenga mazoea ya kufanya hivyo vitu. Nakiri kuwa nimesikia wanaume wengi wakilalamika kuhusu hili kwamba pale wanapochelea kufanya kile mke alichotarajia maneno anayoyapata ni makali sana,na atahesabiwa na yale yote ya nyuma ambayo hakufanya kwa bahati mbaya. Kwa hapa wanawake inabidi tujifunze,hizi lawama ni nyingi sana.
Kiukweli mimi sitakuficha nitakwambia tu kwa vizuri with a romantic tone, mpenzi wangu naomba ukiwa unaoga uweke pazia vizuri basi ili maji yasimwagike nje unaweza kuteleza ukitoga bafuni. Ila Mtambuzi wanaume mmekua mkipokea vibaya sana pale mnapoambiwa ukweli na huwa mnatoa majibu yakukatisha tamaa kabisa. Naomba nikupe mfano hai.....mume amerudi kutoka kazini amefika sebuleni anavua socks anaacha hapo chini anaenda chumbani anavua suruali anaweka chini(na tenga la nguo liko hapo chumbani analijua,analitambua na kuliona) akiingia kuoga anavua c.h.upi anaweka chini. Kweli kaka yangu huyu mtu utaacha kumwambia???!!!! baada ya kumwambia kwa wema kabisa atafanya siku mbili tatu.....mara ataendelea tena vile vile. Sasa hapo mke atakua amekosea nini???!!!!
5.
Hiyo unawezaje kufanya hivyo au sijui nikueleweje lazma itakua imekuja after a very long discussion haiwezekani tu from nowhere mke aanze kusema unawezaje kufanya hivyo?.
Duuuh ila Mtambuzi naona umetuamulia sana wanawake safari hii......sijui yuko wapi mzee Bishanga aje kutusaidia.
Yummy uko sahihi, lakini kumbuka kwamba nilichoeleza sio mkwamba ni formula ambayo mnapaswa nkuifata kama ilivyo, nilichofanya ni kuandika mfano wa namna unavyoweza kucheza na maneno na vitendo kulingana na namna unavyomjua mumeo.............
Kuhusu kuwaamulia wanawake, naomba uniwie radhi, lakini ninayoyaandika ni miongoni mwa malalamiko ya wanaume dhidi ya wake zao, na lengo langu ni kwasaidia wanawake wajue ni kitu gani waume zao wanataka?
lakini pia sijamlenga mtu, yule anayeona anayafanya hayo na kumridhisha mumewe, haimhusu, lakini yule mwenye udhaifu huo, basi ujumbe umfikie.........................................
Aproaching dada yangu ndiyo inayowaponza, inawezekana mwanamke akamwambia mwanaume kwa upole na mapenzi, lakini kama ameanza na kumkosoa kifedhuli hiyo haisaidii kabisa......Kitu ambacho nimegundua kwa wanaume wengi hawapendi kukosolewa/kuelekezwa wanapokosea! Baadhi ya wanaume wanataka wanachofanya wao hata kama ni madudu basi kipite bila kupingwa! Ukimwelekeza hata kwa upole na mapenzi mazito yeye ataishia kua mkali au kukutyson kabisa! Am not married but hua naiona sana hii kitu kwa wanandoa walionizunguka!
1. Kwa mfano, mwanaume hajipendi, mwanamke anapojaribu kuikemea tabia hiyo anakuwa anajenga ukuta mkubwa sana kati yao bila yeye kujua. Inashauriwa, badala ya kumwambia moja kwa moja mumewe kwamba aache kutojipenda, inashauriwa ni vyema akamnunulia mumewe nguo na akizivaa amsifie sana kiasi kwamba mwanaume huyo atajiona kuwa kumbe akivaa nguo za kiwango au mtindo fulani anakuwa katika hali ya kuvutia kupita kiasi. Hapo mwanaume naye atajaribu kununua aina hiyo ya nguo. Kwa wanawake ambao waume zao wana tabia ya kutojipenda kimavazi wanaweza kujaribu hata leo ili wapime matokeo ya ujanja huu.
..........................tafuteni wanaume wa kuzaa nao kisha kila mtu ashike hamsini zake, kwani maumbile hayajui kuoa wala kuolewa, bali yanajua kuzaa basi, kwani hata Mungu alisema "muende mkazaane muijaze dunia" na hakusema muende mkaoane...................
Sashel hilo la kudeka kama watoto hawawezi acha, mi kuna kipindi nilikuwa najiuliza hivi ni makusudi au ni kweli?? nimegive birth to twins, nipo busy na watoto, yaani huwezi amini, ananuna na kulalamika kuwa simjali tena, nimemtelekeza, na mambo kama hayo, so ilibidi nijitahidi akiwepo watoto kwa dada zao, wananyweshana maziwa huko na kubembelezana, mpaka labda husby alale au atoke! ndio nitaendelea na wao!"4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo."
Men! men..tukinyamaza kimya ni shida,tukisema ni tabu..and yes stop acting like a child and you will not be treated like one. :ranger:
Naomba nikupe mfano hai.....mume amerudi kutoka kazini amefika sebuleni anavua socks anaacha hapo chini anaenda chumbani anavua suruali anaweka chini(na tenga la nguo liko hapo chumbani analijua,analitambua na kuliona) akiingia kuoga anavua c.h.upi anaweka chini