Wanawake mijini walemewa vitambi


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
UWEZEKANO wa wanawake wa mijini kupata vitambi ni mkubwa mara mbili ya asilimia 32 kwa miaka kumi ijayo tofauti na wa vijijini kwa asilimia 12 katika miaka hiyo, imeelezwa.

Hata hivyo hali ya mama na mtoto kwa sasa ni bora, licha ya kujitokeza tatizo la vitambi na karibu matatizo yote yanayohusu ustawi wa mama ni makubwa zaidi kwa wanaoishi vijijini kuliko wa mjini.

Hayo yalielezwa na Mratibu wa Elimu ya Awali kutoka Idara ya Elimu ya Msingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Clarence Mwinuka, Jumatano iliyopita wakati akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi minane.

Mratibu huyo alikuwa ni miongoni mwa wawezeshaji wa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini, ambayo yalihusu hali halisi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto Tanzania.

Alisema moja ya sababu kubwa za wanawake wa mjini kuota vitambi ni matumizi ya vyakula vya aina mbalimbali bila kuzingatia mazoezi ya mwili, tofati na wa vijijini ambao wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za uzalishaji mali.

Alisema utafiti uliofanyika miaka ya karibuni na Idara hiyo kushirikiana na baadhi ya taasisi na makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya watoto, ambapo wanawake wa mijini wanapaswa kufanya mazoezi ya viungo, ili waondokane na vitambi.

Hata hivyo, alisema utendaji mbovu, malezi, makuzi na maendeleo ya watoto wadogo, ni kutokuwa na bajeti mahususi kwa ajili ya watoto, kukosekana mpango wa utekelezaji na mwongozo wa viwango vya huduma bora.

Kwa mujibu wa Mratibu huyo, watoto nchini wako katika hatari ya unyanyasaji, ukatili na uonevu, kutokana na kukosekana sheria ya kulinda mtoto inayotekelezeka na kuwa wanawake wamekuwa na sauti ndogo katika uamuzi wa mambo yanayowahusu.

Mratibu huyo alisema umuhimu wa lishe kama msingi wa makuzi bora bado haujatambuliwa ipasavyo nchini, ambapo matatizo yanayotokana na lishe duni kwa watoto wenye umri wa miaka chini ya mitano, ni udumavu kwa asilimia 37.7 na uzito mdogo asilimia 21.8 na ukondefu asilimia tatu.
 
Nyamayao

Nyamayao

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2009
Messages
6,969
Likes
30
Points
145
Nyamayao

Nyamayao

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2009
6,969 30 145
kijana leo naona umeamua copy& paste....
 
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2008
Messages
2,720
Likes
34
Points
145
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2008
2,720 34 145
...hii kali! baba kitambi, mama kitambi
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Mmh kweli kabisa.Hivi hakuna dawa za kichina za kupunguza hivi vitambi?
 
Jeni

Jeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2008
Messages
200
Likes
6
Points
35
Jeni

Jeni

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2008
200 6 35
Bujibuji upo jamani vitambi hivyo
 
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
kijana leo naona umeamua copy& paste....
naumwa man nipo kwa Bed but nimeona wanajamii tuhabarishane habari za leo magazetini!
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,376
Likes
1,302
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,376 1,302 280
noma tupu hii sasa
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
18,312
Likes
6,051
Points
280
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
18,312 6,051 280
Mmh kweli kabisa.Hivi hakuna dawa za kichina za kupunguza hivi vitambi?
Kama yule wa kupaka alipaka na vikaongezeka ukubwa bila kutegemea........ hii ya kupunguza kitambi si UTAONDOA TUMBO KABISA......!!!!!!
 
Z

Zion Daughter

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2009
Messages
8,937
Likes
70
Points
145
Z

Zion Daughter

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2009
8,937 70 145
Vitambi ni janga la kitaifa !
Inabidi tumuulize siri ya urembo Mustafa Hassanali.
 
Rubi

Rubi

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Messages
1,622
Likes
52
Points
145
Rubi

Rubi

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2009
1,622 52 145
na hasa kwa foleni za dar kutwa unakaa kwenye daladala au gari masaa kwenda massa kurudi ofini ukae ukitoka bado pengine utafute vya kukaangaza ukifika nyumbani kula kuangalia tamthilia ulale uamke saa kumi kujiandaa kwenda kazini mazoezi saa ngapi na vitambi haviwezi kukosekana.

mwanamke wa vijijini hana vya kukaangiza, muda mwingi yuko shamba au kujitafutia kipato hana muda wa kuangalia tv maana hata umeme hakuna yeye na redio inatosha, kitambi kwake ni nadra
 
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2008
Messages
5,310
Likes
819
Points
280
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2008
5,310 819 280
Diet ya mjini ni mbovu sana kusema ukweli, na ukiwa na diet mbovu mazoezi hayatakupeleka kokote.
Chipsi, Zege, Kuku wa kukaanga, ndizi, maandazi, vitumbua n.k vyote deep fried!
Kisha tunashushia kwa Soda na Bia! Sasa hapo vitambi vitakosekana tena? Na watu wanavyozidi kupata hela ndo lifestyle disease lazima ziongezeke, muda si mrefu tutakuwa na watu wa 300Kg kama Marekani.
 
RayB

RayB

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2009
Messages
2,754
Likes
94
Points
145
RayB

RayB

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2009
2,754 94 145
Ila vitambi vya wanawake navyo ni issue, sasa inakuwaje pale ambapo baba anacho na mama anacho si inabidi wawe selective sana ktk methodology ya yale mambo?
 

Forum statistics

Threads 1,251,233
Members 481,615
Posts 29,763,433