Nimekuwa nikipita sana JF kama Guest,lakini shida niliyonayo imenifanya leo nijiunge na JF maana mawazo ya members humu jukwaani yamekuwa yakinisaidia sana japo nilikuwa napita kama mgeni.
Nina mdogo wangu kajifungua Dec2012 kwakua alijifungua kwa kupasuliwa waliniomba na Mumewe nije nimsaidie kwa hizi siku za mwanzo. Juzi limetokea tatizo mdogo wangu kapata taarifa rafiki yake wa karibu kajifungu na inasemekana mototo ni wa huyo mume wake, dogo mwanzo aligoma kuamini kwa sababu aliamini huyo dada ni rafiki yake na zaidi ya hapo huyo ndo alimfanya afahamiane na huyo mume na mwanzo alikuwa anamsifia sana amepata mume mzuri. Leo kaamua kuvunja ukimya kamuuliza mumewe mume kakiri ni kweli kazaa na huyo anaeitwa rafiki. Basi toka saa tisa mchana jana mpaka muda huu dogo yupo chumbani na mwanae, shemu yupo hapa amewasha Tv ambayo sina hakika kama anaangalia maana sijjawahi muona asubuhi kama kaamkia TV.chakula nilichooandaa usiku asubuhi nimekuta hakijaguswa na mtu. Hivi nimemtumi sms dogo aamke apate chochote maana akishindana na huyu jamaa atakufa kwa njaa na hivi ananyonyesha,Mgeni mimi nashindwa hata nifanye nini kumsaidia mdogo wangu.ingawa naona yupo katika wakati mgumu sana. Natamani nisingekuwepo kushuhudia haya.
Wanawake kwa nini hatupendani? Unazaa na mume wa mwenzio ukifikiria nini? Kama anakupenda kwa nini hakukuoa maana alikufahamu kabla hata ya huyo mwenzio. Alaf unajiita ni rafiki urafiki gani huo wa kuumizana? Unawaza nini? Na endapo ukafanikiwa ndoa ikafa utaingia wewe?na ukiingia unafikiri kweli utakuwa na amani?wanawake tunajitesa wenyewe maana ninaamini wewe unaezaa na mume wa mtu huna raha yoyote. Na huyo mwanaume hawezi kukuamini kama umeweza kumsaliti unaemwita rafiki lazima atakuwa na wasiwasi na wewe kuwa hata yeye utamzunguka, kama unafurahia ndoa ya mwenzio iyumbe/ife kwa ajili yako ni dhambi, hata kama umetongozwa au umejitongozesha Mume wa mtu ni laana, wamama tusipeane shida.