Katika pita pita zangu katika hii miradi mikubwa ambayo zabuni hupewa wachina au nchi yoyote ile apart from Tanzania sijawahi kubahatika kuona engineers wanawake...
Sisemi kwamba hawapo ila binafsi sijawahi kuwaona, kwa mfano huu mradi wa flyover ya ubungo naishia kuona wachina wa kiume tu, sijawahi kubahatika kuona wachina wanawake wapo site wakisimamia kazi kama wachina wa kiume. Je ni mfumo dume kwamba wachina wanawake hawapewi kipaumbele katika miradi kama hiyo?!
Pia katika haya makorokoro ya kichina, wote ninaoona wanazunguka na magari kuchukua hela ni wachina wa kiume tu. Inamaana haya mataifa makubwa ya nje yanayokuja nchini kwetu hayadhamini gender equality au wanawake hawawezi kusimamia miradi mikubwa mikubwa kama ya standard gauge, flyovers etc?!
Ni maoni yangu, nawasilisha