BAI SM
Member
- Nov 16, 2010
- 49
- 33
Kumekuwa na kelele kwa siku nyingi kutoka kwa viongozi CCM kwamba CCM ni chama sikivu na imejitahidi kuleta maendeleo katika nchi, kama unakumbuka ndugu mwana JF, kuna wakati CCM ilianzisha vipindi kwenye TV na RADIO kuonesha maendeleo yalioletwa na chama hicho, na wakawa wanapita mijini tu wakionesha mambo machache machahe bila kuonesha upande wa pili wa maisha kule vijijini.
Joyce Kiria kupitia kipindi chake cha wanawake LIVE ameanza angalau kuonesha Watanzania walio wengi walioko vijijini wanavyoishi maisha ya taabu.
Kipindi ambacho kinaendelea leo pamoja na kwamba anaonesha mambo ya wanawake lakini ni wazi anaweka wazi maisha ya watanzania walio wengi wanavyoishi kama wako jehanamu.
Naamini kwa kipindi hiki ambacho Joice ameamua kuonesha uhalisia wa maisha ya mtanzania kitawapa wakati mgumu wa kutosha watu kama akina Mwigulu ambao kazi yao si kutafuta namna ya kutatua matatizo ya Mtanzania isipokuwa kupambana na watu kama akina Slaa na CHADEMA.