Wanawake kwenye siasa msilete ubaguzi

Wanawake kwenye siasa msilete ubaguzi

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
373
Reaction score
467
Kwamba tunataka usawa wa kijinsia,wanawake na wanaume wote sawa linapokuja swala la uongozi .

Ikitokea mwanamke akawa kiongozi anahaki ya kukosolewa Kama mwanaume haiwezekan tukisema kuwa kiongozi fulani hawezi au uongozi umemshinda huku tukiwa na hoja thabiti na dalili za wazi ,badhi ya wanawake wanakimbilia kumtetea kwa kutumia kigezo kwamba eti huyu mwanamke au anakosolewa kwa sababu ni mwanamke.

Hakuna kiongozi anaechukiwa kwa sababu tu ni mwanamke ndani ya Tamzania watu tunataka usawa na maoni ya watu yasipigwe nyundo Kama mtu hawezi uongozi hawezi tu hata iweje.

Kisitumike kigezo kuwa ule uwanawake wake uwe ndio sababu ya kuonewa huruma hata Kama anavurunda au anafanya Mambo ya hovyo kwenye Taifa.

Tuseme kweli baadhi ya wanawake wanajibagua wenyewe ,mwanamke na mwamume ni sawa tu katika uongozi na tunatakiwa tuwapime kwa kipimo sawa tusilete ubaguzi Kama hujui hujui tu uongozi ni karama.

Hatutaki huruma ya ujinsia ktk kuleta maendeleo ya nchi inatakiwa wanawake wajikubali na ikitokea ,akapewa fursa mwanamke mwenzao ya kuwa kiongozi akiboronga basi wanawake wawe ndio wakwanza kupaza sauti na sio kusifu tu hata Kama anawaharibia wanawake wenzake.

Ukiwa kiongozi ni kiongozi wa watu wote hauongozi wanawake tu nchi au serikali sio kikundi Cha upatu au kitchen part Kama mtu akijiona hana uwezo wa uongozi au maji yamezidi unga au madaraka yamemzidi kimo aachie ngazi mstafute huruma ya kijinsia kwa kutumia propaganda.

Ujumbe wangu huu makhsus kwa kinamama wote wapenda maendeleo kwa siku ya mama duniani, tusijibague katika swala la uongozi wanawake na wanaume ni sawa tofauti inakuja katika weledi na uwezo binafsi wa mtu katika uongozi husika.

Asiyeweza aambiwe ukweli kuwa huwezi.

Tusimtetee kisa mtu anayetuuza kisa tu mwanamke, anayeboronga aambiwe ukweli Kama mama au Bibi au shangazi eeh huko unapotupeleka sio asitumie kichaka cha jinsia kujifariji na kupofusha watu fikra na maoni yao.
 
Defensive ya ujinsia ilianza hapa; 'mimi ni raisi mwenye jinsia ya kike'!
 
Back
Top Bottom