Wanawake kwa nini hampendani katika hili?

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,314
Wanawake (walioolewa na ambao hawajaolewa) nawashauri muache kuoneana wivu na kuchukiana kwa kutupigania wanaume.

Inaeleweka kabisa sisi wanaume tuko wachache nyie mmejaa telee hivyo mwanaume mmoja kumiliki wanawake kadhaa ni sahihi kwani hata Biblia takatifu inazungumzia hili jambo.

Upande wetu sisi wanaume hatunaga tatizo baina yetu kabisa, tukijijua tumegongana kwa mwanamke mmoja basi mmoja wetu huondoka kiroho safi na kwenda kutafuta chimbo lingine kwani mmejaa telee.

Upande wenu nyie wanawake ndio kuna tatizo kubwa sana. Hampendi kabisa kushirikiana wakati mnajijua kabisa mko wengi kuliko sisi wanaume.

Ewe mwanamke jiulize ukikataa mwanamke mwenzio ajibanze kwa mwanaume wako ataenda wapi ambapo pako wazi? Hamna pa kwenda kwa maana pote pameshajaa.

Isaya 4:1 inasema "Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu."

Hivyo wanawake acheni kuleta taharuki kwenye jamii mnapoona mwanaume anamiliki michepuko kwani nyakati alizosema Isaya ndio hizi. Sisi wanaume ni nani hasa hadi tupingane na maandiko matakatifu?

Shida iko kwenu nyie wanawake kwani mnakataa kuyaishi maandiko matakatifu. Tukiishi kwa kufuata maandiko dunia itakuwa sehemu nzuri mnooo.

Mbona wenzenu upande wa Islam hawana tatizo hata mwanaume aoe wanawake 4? Sababu wanajua hiyo ni stara, wanapenda wanawake wenzao wastiriwe.



Screenshot_20190819-151814.jpg
 
Back
Top Bottom