Wanawake kuita waume zao Mr

Wanawake kuita waume zao Mr

lovebitelol

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
964
Reaction score
972
Habarini za leo wakuu.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja juu hili jina wanalotumia wanawake waliiolewa siku hizi (wa kidigitali).

Imezuka tabia ya wanawake walioko kwenye ndoa wakati wa kumtaja mume wake au bwana wake kusema Mr. Mfano umemkuta mwanamke sehemu amekaa then unamuliza kulikoni mbona uko hapa anakujibu " namsubiria Mr."

Sasa hapo unajiuliza kwanini asiseme anamsubiri mume wake au bwana wake kama ilivyokua zamani? Kwani mtu kusema mume wangu au bwana wangu inaleta tafsiri gani kwa watu? Hadi mtu amuue kusema Mr? Mbona sijawahi kuona mwanaume akisema niko na Mrs au Mrs yuko nyumbani na nk.

Nadhani wanawake wa siku hizi wako kimachale au kimtego zaidi. Yaani anaona akisema Mr. inaondoa maana kidogo kuliko akisema mume wangu. Ukiona mke wako anakutaja kwa watu kama Mr. ujue hauna thamani kihivyo anakuchukulia powa tuu.
 
Mbwembwe tu halaf unaweza kukuta huyo mr wiki nzima ndani hawasemeshani ila huku nje mashauzi
 
wanawake wa siku hz minara... anajua akisema Mr tayar kajiweka salama sababu hajakupa jibu la direct..coz Mr anaweza kuwa bwana, bosi, rafik, au hata dalali.. kwahiyo unashindwa kumwona hajatulia..!
 
wanawake wa siku hz minara... anajua akisema Mr tayar kajiweka salama sababu hajakupa jibu la direct..coz Mr anaweza kuwa bwana, bosi, rafik, au hata dalali.. kwahiyo unashindwa kumwona hajatulia..!
Yessss
 
Habarini za leo wakuu. Bila kupoteza muda niende moja kwa moja juu hili jina wanalotumia wanawake waliiolewa siku hizi(wa kidigitali).

Imezuka tabia ya wanawake walioko kwenye ndoa wakati wa kumtaja mme wake au bwana wake kusema Mr. Mfano umemkuta mwanamke sehem amekaa then unamuliza kulikoni mbona uko hapa anakujibu " namsubiria Mr." Sasa hapo unajiuliza kwanini asiseme anamsubiri mme wake au bwana wake kama ilivokua zamani? Kwani mtu kusema mme wangu au bwana wangu inaleta tafsiri gani kwa watu?hadi mtu amuue kusema Mr? Mbona sijawahi kuona mwanaume akisema niko na Mrs au Mrs yuko nyumbani na nk.
Nadhani wanawake wa siku hizi wako kimachale au kimtego zaidi. Yaani anaona akisema mr inaondoa maana kidogo kuliko akisema mme wangu.
Ukiona mke wako anakutaja kwa watu kama mr ujue hauna thamani kiihivo anakuchukulia powa tuu.
Mbona mimi wanawake,wanaume,wazee,vijana wananiita Mr. RRONDO?
 
Lovebitelol, hata wakati wa kutongoza, ni rahisi kusema "I love you" kuliko kusema "nakupenda".
 
Back
Top Bottom