Wanawake: Kama una mtoto ukiolewa usiende nae

Wanawake: Kama una mtoto ukiolewa usiende nae

Halafu hata haisumbui kuwalea.Binti yangu (japo sijamzaa mimi) nilimuahidi akifaulu form 4 namnunulia simu na leseni ya kuendeshea gari (maana kuna kigari nilichoanzia maisha kipo kipo tu).Matokeo yametoka kaniumbua vibaya mno,nimemuambia simu mpaka chuo kikuu ila gari ndio nipo kumfundisha ili nisimvunje moyo.
Mara nyingi wanakuwaga na akili sana, hata huyu wa aunt yangu alifaulu vizuri sana, ana maisha mazuri sana sasa hivi eti ndiyo baba yake anamtafuta. Mapenzi yake yote yapo kwa baba aliemlea.
 
Damu ni Nzito kuliko maji, ukweli mchungu huu, Single mother kiuhalisia ni tatizo hata aolewapo yani kuna siku atakusema vibaya juu ya huyo mtoto mpaka ujione zuzu, Changanya na mishe za kupasha kiporo na baba aliezaa nae but ni kujitwika mizigo isiyo na ulazma labda babake awe kafa, Mimi Yatima nitamlea kwa moyo wote pengine kuliko mwanangu wakumzaa
 
Ukatili ni mwingi sana ila idadi kubwa ya wanawake ndio wanaoongoza kwa kufanya ukatili tena kwa watoto waliowazaa wenyewe.
Aina ya ukatili unaofanywa na wanaume mwingi unahusiana na masuala ya ulawiti na mapenzi kwa watoto wa kike wa wake zao ama watumishi wa kazi.
Nimeshuhudia wanawake wanawachoma moto watoto wao wa kuzaa wenyewe kisa amekomba mboga ama kaiba kitu. Lakini rate percentage mwanamke ni katili kuliko mwanaume na nimefikia hatua yaani nawaogopa wanawake maana niliyoyashuhudia yanatisha.
Wanaume ugonjwa mkubwa uko chini tu basi na matukio yao mengi ni hayo nao ni wachache ukilinganisha na wanawake.
La msingi tuheshimiane ktk ndoa zetu.
 
Hata huko unakomuacha sio salama pia, ni Mungu tu apitishe mbali maana huo ni ushetani tuu.
Wangapi wanawabaka watoto wao wa kuwazaa?? Tuwaombee tu hawa wanaume maana kwa akili zetu hatutaweza
 
Mara nyingi wanakuwaga na akili sana, hata huyu wa aunt yangu alifaulu vizuri sana, ana maisha mazuri sana sasa hivi eti ndiyo baba yake anamtafuta. Mapenzi yake yote yapo kwa baba aliemlea.
Ni kweli kabisa,ni kama Mungu anakua upande wao 100%. Nawaombea wafanikiwe ili waje kuwa na familia isiyo na kumbukumbu ya malezi mabovu kutoka kwa wazazi.
 
Damu ni Nzito kuliko maji, ukweli mchungu huu, Single mother kiuhalisia ni tatizo hata aolewapo yani kuna siku atakusema vibaya juu ya huyo mtoto mpaka ujione zuzu, Changanya na mishe za kupasha kiporo na baba aliezaa nae but ni kujitwika mizigo isiyo na ulazma labda babake awe kafa, Mimi Yatima nitamlea kwa moyo wote pengine kuliko mwanangu wakumzaa
Kulea mtoto wa kambo ni sawa na kulea mtoto wa kaka,dada,shangazi,binamu au mdogo wako.Mwanamke kuchepuka na mwanaume alie zaa nae ni sawa na kuoa mwanamke ambaye hakuzaa ila alikua na wapenzi aliokua anawapenda sana kabla yako wewe.Aliolewa na wewe kwa sababu alidanganywa na wengi au umri umeenda.Wale kabla yako wakirudi watapasha tu kama huyo unaemsema single mother.Maisha ya ndoa sio ya kujifunzia kijiweni,muombe Mungu akupe mke mwema.
 
Kichwa cha chini kinapochukua nafasi ya kufikiria badala ya kichwa cha juu, mwili na akili vyote vinakosa nguvu ya act kama binadamu wa kawaida, na mtu anageuka kuwa kiumbe cha ajabu.
 
Baba wa namna hiyo hashindwi kumlala mtoto wake wa kumzaa.
 
Wanaume wamekua zaidi ya wanyama jamani!!! Yaani pepo la ngono limewatawala. Siku hizi hamna cha kumuamini baba wa kambo wala ndugu wa kiume! Watoto wanaharibiwa sana. Ata hawa mashoga wengi walianzishwa na wajomba na baba wadogo.
Ni kuwaweka kwenye maombi watoto wako na kua makini saana
 
Ungetusimulia tu hadithi halafu watu wakapima wenyewe.
Mbona wapo watu kibao wamelea watoto wa kambo fresh tu, halafu je kama mtoto akiwa wa kiume, Naye ana weza bakwa?
Halafu hao watoto wasiende nao waweke wap?
Ungesema at least kina maza wawe makini kwenye mazingira kama hayo.

Tukio moja lisijumlishe watu wote.
Kesi za hivi zimezidi sana wakati huu!!! Na si kwamba ndo zimeanza tokea saivi ila uwepo wa mitandao ndo inatufumbua macho.
Mi sidhani kama kutokwenda na mtoto ni suluhisho!!! Mtoto akikua hatamuelewa mama yake eti nilikuacha kwa bibi kwasababu nilikua nakwepa baba wa kambo asije akakubaka!!! Ata mimi siwezi muelewa mama wa hivyo, eti aniache akaolewe huko na awe na familia nyingine!!! Ntaona hakunipenda na hakutaka tu kuishi na mimi.
 
Ata hawa mashoga wengi walianzishwa na wajomba na baba wadogo.
Ni kuwaweka kwenye maombi watoto wako na kua makini saana
Ni malezi, usije ukajaribu kusema eti haya kalale na baba ako mdogo, cjui kalale na mjomba ako, hata nyumbani watengee vyumba watoto na usiku una piga doria. epusha mtu yeyote mkubwa kumzoea zoea mtoto wako.
Siku hizi mambo yamekuwa si mambo.
Kulea mtoto miaka hii ni kazii
 
Kesi za hivi zimezidi sana wakati huu!!! Na si kwamba ndo zimeanza tokea saivi ila uwepo wa mitandao ndo inatufumbua macho.
Mi sidhani kama kutokwenda na mtoto ni suluhisho!!! Mtoto akikua hatamuelewa mama yake eti nilikuacha kwa bibi kwasababu nilikua nakwepa baba wa kambo asije akakubaka!!! Ata mimi siwezi muelewa mama wa hivyo, eti aniache akaolewe huko na awe na familia nyingine!!! Ntaona hakunipenda na hakutaka tu kuishi na mimi.
Pap
Siku za jumapili uwa unatema point tupu, [emoji1]
Au huwa unaenda kwa gwajima!!?
 
Ni malezi, usije ukajaribu kusema eti haya kalale na baba ako mdogo, cjui kalale na mjomba ako, hata nyumbani watengee vyumba watoto na usiku una piga doria. epusha mtu yeyote mkubwa kumzoea zoea mtoto wako.
Siku hizi mambo yamekuwa si mambo.
Kulea mtoto miaka hii ni kazii
Kazi tena si ndogo!
 
ni tabia ya kishenzi tu ya baadhi ya wanaume wasiojitambua kiakili.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom