Wanawake-heri mimi sijasema………….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake-heri mimi sijasema………….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Dec 19, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba, wanawake huwazidi wanaume katika kiwango cha kujilimbikizia vijidudu vya maradhi kwenye maeneo yanayowazunguka, ikiwa ni pamoja na meza zao za kazi ofisini, simu zao na kompyuta wanazotumia. Vile vile makabati yao ya kuwekea vitu ofisini au nyumbani, pamoja na vitu vyao binafsi kwa ujumla.

  Utafiti huo uliofanywa na profesa Charles Gerba wa chuo kikuu cha Arizona nchini Marekani umebaini ukweli huo kwa uwazi zaidi kuliko tafiti za awali. Gerba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya udongo, maji na mazingira, alichunguza na kupima zaidi ya maofisi 100 kwenye chuo kikuu cha Arizona, New York, Los Angeles, San Francisco, Oregon na Washington DC, katika utafiti huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 52 chini ya ufadhili wa kampuni ya Clorox.

  ‘Niliamini kabisa kwamba kutokana na hali ya wanaume kutokuwa nadhifu na wasiojijali sana kama wanawake, bila shaka wangekuwa wenye kubeba viini na vidudu zaidi vya maradhi kulinganisha na wanawake,' alisema Gerba.

  Lakini hali ni tofauti kutokana na wanawake kuwa na kawaida ya kushirikiana kwa karibu zaidi na watu wengine na hasa watoto na kuwa na tabia ya kupenda kuweka vyakula kwenye meza zao za kazini. Tatizo jingine ni vipodozi. Dhana ya mwanzo ya Gerba ilitokana na ukweli kwamba meza za wanawake siku zote huonekana nadhifu na zilizopangiliwa kulinganisha na za wanaume, lakini mabaki japo madogo sana ya vyakula, vipodozi na mafuta ya kujipaka ni ya kawaida kwenye meza zao na hivyo kuwa kichocheo kikuu cha ufugaji wa viini vya maradhi..

  Mikoba ya kubebea vipodozi nayo huvipatia viini na vidudu hivi makazi ya usalama kwao, pamoja na simu na mikoba ya kubebea vitu vyao vingine, na madroo ya kwenye meza. Vyakula vinavyohifadhiwa kwa muda kwenye meza za maofisini navyo huvutia na kuhifadhi wadudu, na tabia hiyo ni ya kawaida zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Katika utafiti wake, Gerba aligundua kwamba, asilimia 75 ya wanawake wanakuwa na vyakula kwenye meza zao za maofisini. Hiyo ni karibu kote duniani. Wanaobeba vyakula na kwenda navyo ofisini ni wanawake zaidi. ‘Kwa kweli nilishangazwa na kiasi kikubwa cha vyakula nilivyokuta vimehifadhiwa kwenye meza za wanawake,' alisema mtafiti huyo.

  Kwa upande wa wanaume Gerba aligundua kwamba sehemu ambayo husaidi kuzalisha viini vya maradhi ni kwenye pochi za wanaume ambazo kwa kawaida huwekwa kwenye mifuko ya nyuma ya suruali ama kwenye makoti ya suti, lakini pamoja na ukweli huo bado wanawake ndiyo wenye kuzalisha vijidudu vya maradhi zaidi


  Msijenitoa macho mie:
  http://www.infectioncontroltoday.com/news/2007/02/germs-working-overtime-especially-at-women-s-desk.aspx
   
 2. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kiongozi ! Wanachotakiwa wakushukuru kuwafungua macho, mi Mwanaume sio mlengwa hapa.
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wanaume pia ni walengwa, kwani nao pochi zao zimetajwa kuwa ni mazalia ya vijidudu vya maradhi..............kinachotutofautisha na wao ni uwiano tu................
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Hizo ni tafiti za kizungu.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kweli eh! Unajidanganya aisee........... hivi wewe hufanyi kazi ofisi moja na kina dada? Je, huwaoni na viji Bites kwenye mikoba yao?
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Na mwisho wa siku tunawapaka vidudu usiku, laa!
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Shikamoo baba,
  Dah!huyu mtafiti mbona ameniongelea mm hapa,
  Hapa nilipo nakunywa chai hapa mezani kwangu,
  Na siku zote huwa nakuja na juice yangu kutoka hm,
  Bila kusahau vitafunwa huwa nakuja navyo kila siku,
  Basi km ni mavidudu mie nayatengeneza mengi lol!
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  wewe ni He kumbe?
   
 9. molely molly

  molely molly JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 317
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dat true kaka hii mambo dada zetu wanazo :shock:
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Najua uko kwenye mikakati ya kujifunga mkanda ili ujinunulie vipodozi....................... Si unajua mambo ya kujikwatua!
   
 11. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Haaa haaa haa,
  Hapa umenionea baba,
  Unajua kbs mwanao fani hiyo sina,
  Napenda tu juice niliyotengeneza mwenyewe,na mikate ya ofic kila siku inachosha baba.
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndio maana unajinunulia mkate wako wa Boflo kwa huyo Mpemba hapo jirani na kwako........................
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Leo ukija kutoka huko hakuna kuhag sijui kiss na kitandani hakuna kugusana!
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mmmmhh. . !
   
 15. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Heheh sasa hapo sijui solution ni nini aisee!!
   
 16. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umemaliza!??
   
 17. v

  valid statement JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kuoga kabla na baada ya kulala/kulalana. Ni lazima. Utavipaka wapi sasa?
   
Loading...