Wanawake hayo yote kwa ajili ya nani?

Wanawake hayo yote kwa ajili ya nani?

kadovela

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Posts
471
Reaction score
679
Unakuta mwanamke ni mama tu wa nyumbani kaolewa na mumewe na anapendwa sana asubuhi kama ilivyo wajibu anaamka mapema anamuandalia maji ya moto ya kuoga mumewe.

Mumewe anaamshwa anakwenda bafuni kuoga anatoka kuoga anakuta nguo imenyooshwa anavaa anakaribishwa kifungua kinywa na mkewe anapata chai kabla ya kuanza safari ya kwenda kazini anamfuata mkewe kwa tabasamu anamkumbatia na kumbusu kwa huba na kumtakia mkewe abaki salama.

kumbuka haya yote yanafanyika wakati huyu mke alikurupuka asubuhi bila kupiga mswaki,kuoga wala kunawa uso ili amuweke sawa mumewe aende kazini, uwa najiuliza baada ya hapo huyu mwanamke kushinda kujipodoa na kujikoboa full ma make up, na urembo wa gharama kubwa yote anafanya kwa ajili ya nani?

Hivi kufanya usafi wa mwili na kujiweka sawa bila maurembo ya gharama haiwezekani? hayo yote kwa ajili ya nani wakati mumeo hata katika muonekano wa kuamka asubuhi bado anakupenda na kuthamini uwepo wako kwake, nauliza hayo yote kwa ajili ya nani?
 
Mkuu ilikuja thread juzi kati tulipigwa virungu balaa. Yan wao hawataki kisikia kabisa. Wanacho amini wao ndio hicho. Kumbe wanapoteza mvuto wao ma uhalisia wao
 
soma maandiko mkuu yakutoe upumbavu mwanamke amefananishwa na pambo kwenye bible na maana ya pambo ni kitu ambacho kinakupa furaha muda wote ukikizama kwa uzuri wake

iv utaridhika kula wali nyama kila siku??? nooooo siku nyingine inabidi ule ugali ule ndizi na nk, hivyo hivyo kwa wanawake wanatakiwa kubadilika (kujipamamba) ili wewe mume uweze kumfurahia na mkumuona mpya kilasiku sasa kama wewe hutaki mkeo ajirembe basi pamaba na hali yako but unatakiwa kujua anafanya yote hayo ni kwaajili yako hata yeye akipendeza sifa zitakuja kwako
*virginboy*
 
Mambo yakujigeuza mdori koma Kabisa nyie wanawake wengine mpaka kujichubua nani kakwambia weupe ndo uzuri siendi mie
 
Sasa akiamka akaanza kuoga yeye na kujipodoa atamaliza SAA ngap? Akuandae wewe?

Akijipodoa wakati haupo ukirudi si utamkuta utamwangalia.

Anyway hongera kwa kupata mke anayekujali kiasi hicho cha kuamka mapema kukuchemshia maji na chai.

Wengine hivyo vitu ni ndoto....
 
Kichwa cha habari kingekuwa
"Hivi mama haya unafanya kwa ajili ya nani?
 
Nashukuru Mungu mke wangu gharama anazotumia yeye ni kutengeneza nywele tuu hayo mavipodozi hata hana time nayo.
 
Daaa kiukweli mimi mke wangu lazima aje kupendeza. Akijiweka kihasara hasara kama anavyoshauri mtoa thread nitamchoka mapema mno
 
Sasa akiamka akaanza kuoga yeye na kujipodoa atamaliza SAA ngap? Akuandae wewe?

Akijipodoa wakati haupo ukirudi si utamkuta utamwangalia.

Anyway hongera kwa kupata mke anayekujali kiasi hicho cha kuamka mapema kukuchemshia maji na chai.

Wengine hivyo vitu ni ndoto....
Wanaume wa jf kwa kujifanyaga wake zenu hawawajali[emoji57]
 
Kwa ajili yako ukirudi,.ww unataka unikute ulivyoniacha asbh!? mweh si utakuja humu tena na nyuzi zingine kunisimanga!?
 
Back
Top Bottom