Katika ubora wake..Huyo ndiye Mama Samia.
Maelfu ya wananchi wakiwemo wanawake wamejikuta wakitoa machozi wakati wa mapokezi ya Mama Samia.Hata hivo Mama Samia amewaahidi kuwa serikali yake itaweka mkazo katika kuboresha huduma za Maji na Afya mkoani Geita ili kupunguza adha za wanawake.
Maelfu ya wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita leo
Samia na CCM ndio waliowaliza wananchi na maovu yao, bila aibu wanakwenda kuwaomba kura ili waendelee kuwaliza.
Safi saana. Wanawake wenzake wanalia machozi kuona jinsi ambavyo mwanamama mwenzao ameamua kuwahadaa tena. Wamekumbuka ahadi za ccm kuwa hazitekelezekiiiii
Nyomi za kampeni tuziweke pembeni na mbali, kwani haziwakilishi uhakisia wa ushindi. Kama wewe ni mtu makini, tazama umri wa watu wanaohudhuria mikutano hiyo na matendo yao. Hiyo itakupa picha halisi ya nani ni mpiga kura wa kweli. Mikutano ya kampeni iliyojaa ushabiki ni vurumai na uhuni mtupu ya watoto wa mjini, watu wenye hekima na busara hawahudhurii.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Unafikiri ndiyo lowasa anatumia mapepo, fotoshop, kuhonga watu hela wazomee, kutembea na watu toka arusha, mnadhani sisi hatujui mbinu zenu? CCM lazima ishinde, taifa haliwezi kukabiziwa kwa mwizi, jambazi, na fisadi