Wanawake CCM sasa wasakamana

Wanawake CCM sasa wasakamana

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
Na Cynthia Mwilolezi 4th December 2012

Makundi bado yanakitafuna Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama hicho mkoa huo, Flora Zelote, kudaiwa kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige, kuwa misaada aliyoitoa wiki iliyopita ina lengo la kutaka ubunge kupitia jumuiya hiyo mwaka 2015.

Hatua ya Zelote ya kumshambulia Magige inafuatia kitendo cha mbunge huyo wiki iliyopita cha kutoa msaada wa baiskeli 20 kwa walemavu zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni nane.

Mbunge huyo kupitia Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM), alitoa msaada huo baada ya kuzindua taasisi yake ya kusaidia vijana, wanawake na watoto ijulikanyo kwa jina la "Chatherine Foundation Development" yenye makao yake makuu jijini Arusha.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Arusha kilichofanyika Arumeru Novemba 30, mwaka huu, zinasema kuwa Zelote ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Musa Wilaya ya Arusha, alimshambulia Magige na kuwaeleza wajumbe kuwa mbunge huyo hana jipya kwani misaada anayotoa ni ya kutaka kujijenga ili aweze kupata ubunge mwaka 2015 kupitia UWT.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Zelote alisema katika kikao hicho kuwa anamtambua mbunge mmoja tu wa Viti Maalum mkoani Arusha ambaye ni Namelok Sokoine, mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Aidha, habari zinasema kuwa Zelote alihamasisha wanawake kutohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Magige.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa Zelote aliwaeleza wajumbe kuwa hawana sababu ya kuhudhuria kwa kuwa kazi inayofanywa na mbunge huyo (Magige) siyo ya wanawake, bali ni ya walemavu na yeye (Zelote) asingehudhuria kwa sababu hizo.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu ili kutoa ufafanuzi wa kuhusiana na suala hilo, Zelote alithibitisha kutohudhuria katika shughuli hiyo kwa maelezo kuwa ilikuwa ya wenye ulemavu na siyo ya UWT.

Pia, Zelote alithibitisha kusema kuwa anamtambua Namelok Sokoine kuwa ndiye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha.

Hata hivyo, alipoulizwa kwa nini hamtambui Magige kuwa Mbunge wa Viti Maalum, alijibu kuwa hamtambui kwa kuwa anatokana na UVCCM na siyo UWT anayoiongoza.

Kuhusu madai kuwa alisema misaada ya Catherine ni ya kujijenga kutaka ubunge mwaka 2015 kupitia UWT, Zelote alikana kutoa kauli hiyo na kufafanua kuwa alichokisema ni kuwa ilikuwa misaada kwa ajili ya wenye ulemavu na jamii nyingine.

"Kweli ninayemtambua ni mbunge mmoja tu Namelok Sokoine wa Viti Maalum mkoa wetu (Arusha) na siyo mbunge mwingine na nitaendelea kuamini hivyo siku zote, ila kuhusu misaada ya Magige kuwa ni kampeni ya ubunge kupitia UWT siamini hivyo," alisema.

Magige alipoulizwa kuhusu tuhuma za kushambuliwa na Zelote, alithibitisha kuzisikia na kueleza kuwa kutoa kwake misaada ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM kwa jamii inayowazunguka na siyo kampeni za ubunge.

Alisema kwa sasa Rais, Dk. Jakaya Kikwete na ndiye anayemheshimu na kumsaidia katika kutekeleza ilani ya CCM mpaka mwaka 2015 atakapopatikana Rais mwingine.

"Rais ajaye wa mwaka 2015 hakuna mtu anayemjua kwani ni Mungu pekee ndiye anayemjua na kama wao wanaye Rais wao, waendelee kuamini hivyo, lakini hilo kwangu halipo,'' alisema Magige.

Akizungumzia kutaka kuwania ubunge kupitia UWT Mkoa wa Arusha, Magige aliwataka wanawake kusubiri muda ufike ili kila mwenye sifa ya kugombea agombee kwa kuwa ni haki ya kila mwana chama wa CCM.


CHANZO: NIPASHE
 
Hivi bado kuna wanawake wanaota 2015 bado kutakuwa na UBUNGE WA VITI MAALUMU?

Labda hiyo katiba mpya isipatikane.
 
Niko hapa karakata karibu na aiport,kuna lodge inaitw kiceec,kuna wana ccm kadhaa wanapanga namna ya kuihujumu cdm kwenye kila uchaguzi utakao kuja mbele.
 
WIKI mbili baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana, kutua Arusha na kuacha wosia akiwataka wanachama kuwa kitu kimoja, pepo wa kutengana sasa amedaiwa kuanza kunyemelea tena utulivu wa viongozi.

Katika kile kinachodaiwa ni mwanzo wa vita mpya ya kuusaka ubunge wa viti maalumu UWT Mkoa wa Arusha mwaka 2015, Mwenyekiti wa UWT, Flora Zelote, anadaiwa kurusha kombora kwa Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Kikao cha Baraza la Jumuiya hiyo Mkoa wa Arusha, vilisema Flora anadaiwa kurusha kombora la waziwazi lililomlenga Magige.

Chanzo cha habari kilichokuwa ndani ya kikao hicho kilichokutana Novemba 30, mwaka huu Arumeru kilidai Flora alisikika akidai hamtambui Magige kama Mbunge wa Viti Maalumu, bali mbunge anayemtambua ni Namelock Sokoine.

Akithibitisha tuhuma zilizotolewa dhidi yake, Flora, alisema ni kweli alisema hivyo kutokana na hoja alizodai kuwa Magige hatokani na UWT.

“Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha ni Nameloki kwa kuwa ndiye ametokana na UWT, na Magige yeye anatokana na UVCCM,” alisema Flora.

Chanzo chetu cha habari ndani ya kikao hicho kiliendelea kusema pamoja na kurusha kumbora hilo, bado Mwenyekiti huyo alirusha kombora jingine kwenda kwa Magige.

Kombora kwenda kwa Magige lililenga kutuhumu misaada ambayo mbunge huyo amekuwa akiitoa kwa jamii mbalimbali, ikiwamo walemavu na watoto wanaoishi katika mazingita magumu.

Mwenyekiti huyo anadaiwa kusema misaada inayotolewa na mbunge huyo, imekuwa ikilenga kujipanga kwa ajili ya kuwania ubunge kupitia UWT mwaka 2015 na si vinginevyo.

Wiki iliyopita Magige akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, alitangaza rasmi kuzindua taasisi yake ya Catherine Foundation itakayolenga kuwasaidia watu wasio na uwezo.

Katika uzinduzi huo, walemavu 20 walikabidhiwa baiskeli maalumu za kuwasaidia kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, katika kujiingizia kipato, zikiwa na thamani ya Sh milioni sita.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa UWT, akijibu tena madai hayo yaliyovuja kutoka ndani ya kikao chake alipinga kutoa kauli hiyo na kusema shughuli hiyo ilikuwa ni maalumu kwa wenye ulemavu na si UWT.

“Si kweli kwamba nimetamka misaada inayotolewa na Magige ni ya kujijenga kutaka ubunge wa UWT mwaka 2015, binafisi siamini hivyo kwa kuwa ni wazi kwamba misaada imekuwa ikilenga walemavu na jamii nyingine,” alisema Flora.

Kwa upande wake, mwanachama wa UWT, Odilia Abrahamu, akizungumzia mtafaruku huo alidai haamini kama maneno hayo yalitolewa na kiongozi mkubwa wa Jumuiya hiyo.

“Misaada inayotolewa na Magige haijaanza leo wala jana, amekuwa akisaidia Jumuiya ya wanawake, familia zisizojiweza na hata walemavu muda mrefu, leo iweje atuhumiwe anajijenga kwa mwaka 2015,” alisema Odilia.
 
Aibu tupu! Naona hapa ugomvi ni nani anaungwa mkono na kambi ipi! Ninyi wanawake hamjui ni aibu ya hata waume na wazazi wenu kugombana hadharani kwa ajili ya nani ni wanani ndani ya CCM? Ninyi masikini wenzetu mmepata wapi hayo mamilioni ya eti kuwasaidia watu wasio na uwezo. Acheni kuita wenzenu wasio na uwezo. Je! hamjui kuwa mmewasahau mliokuwa nao na waliwapigia kura? CCM ni mahututi amini msiamini!
 
Wanagombea ubunge wa chup... maana hawana uwezo wa kujisimamia. Watakoma maana ni wengi kuliko viti vyenyewe hasa baada ya upinzani kuvinyakua baadhi.
 
Hatutaki viti maalum, hatutaki wabunge wa taasisi, hatutaki wabunge wa kuteuliwa na rais .... tunataka wabunge wanaochaguliwa na wananchi, period.

Na mawaziri, mabalozi na wakurugenzi wa mashirika ya umma, wote wapitishwe na bunge kwanza. Hawa kina mama wanatutia aibu na njaa zao!!
 
Hivi hawa vilaza bado wana ndoto mbovu kama ilivyotajwa!

Hata hawasomi alama ya nyakati kweli!

Acha mvua inyeshe tujuwe wapi panavuja!
 
Wana chadema huyu dada hana nafasi kwetu angalia nguo alizovaa ni bendera ya Chadema. kwanini asivae rangi zao zile za kijani.... ipo kazi bila hat ya kupiga hodi hukaribishwi!!! Catherine Magige1.jpg
 
hawa wanawake wa CCM wanaugomvi wao wa mabwana.
In short hawa wanawake wa CCM hapa arusha wanaongozwa na akili za ngono
 
Back
Top Bottom