Hivi hizi taasisi na vyama vyama vya wanawake tz imekaaje hii;
` WBA - bank ya wanawake Tz`
` WAMA- wanawake na maendeleo`
` KIWOHEDE- Kilimanjaro Women H.... Development.. Mtanisaidia hapo kwenye H wana jf kirefu chake nimesahau`
` MEWATA- Chama cha madaktari wanawke TZ`
` TAWLA - Chama cha sheria cha wanawake tz`
` TAMWA - chama cha waandishi wa habari wanawake tz`
Ipo siku tutasikia wanaunda Jeshi la kinamama Tz. na hii yote ni kuwabana wanaume sijui tumewakosea nini Mungu wangu.
Haya yote wanayafanya ili kwamba wawe na sauti moja katika kuwakabili wanaume katika Yale wanyoamini ya kuwa wanaume wanawanyanyasa ama wanawatenga katika nyanja mbalimbali za kijamii hasa kwenye nafasi za juu kiuongozi na wanasahau ya kuwa hakuna sehemu wanayotengwa kila mtu anaingia sehemu ya kazi kwa qualifications lakini naona kama waangeridhika sana ikiwa wangepewa nafasi za juu za uongozi bila kujali cvs ama uzoefu na vitu vya namna hiyo.ikiwa wanajianzishia vikundi ama jumuiya basi wasizibane sana kwa maana ya gander moja waanzishe jumuiya ambazo zitachanganya jinsia zote ili kama ni kujadili mambo ya kimaisha ama jamii kwa ujumla majdiliano yashindanishe jinsia zote na hata kama ni kutenda kwa maana ya uwajibikaji kuwepo na ushindani ulio sawa
Tangu Mungu anaumba dunia, alimfanya mwanaume kuwa juu na itaendelea kuwa hivyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Ndo maana Biblia inasema Askofu na asiwe mwanamke.
Mambo ya beijing hayo! hata hivyo nawahakikishia hizo taasisi zao nyingi zipo kisiasa zaidi! wakisimama majukwaani wanaongea hao! lkn wakirudi nyumbani heshima na adabu! ni namna flan ya kujitutumua ili basi angalau tujue nawao wapo!
Biblia inasema katika kitabu cha MWANZO,3:16 Mungu alisema hakika tamaa ya mwanamke itakuwa kwa mmewe naye mwanamme atamtawala mwanamke, hili ndilo agizo la Mungu kwa manamke, sasa wajihadhali wasiende kinyume na Mungu wao.
Wanajitahidi kuwa sawa na wanaume lakini wanajichanganya kwamba ni usawa gani wautakao,wakumbuke ya kwamba mungu alikusudia kumwumba Binadamu kama mwanaume na alipokwisha maliza ndipo akaona ni bora ampe huyu mwanamume mtu wa KUMSAIDIA ambaye ni MWANAMKE hivyo baadaye ndipo alipomwumba mwanamke na wala hakuwananisha..