Jamani siyo siri wapo akina dada wao utadhani wameshushwa duniani kupoteza amani za wanaume. Pamoja na wanaume wanamatatizo yao, lakini inapofikia mke yeye ni kuendeleza ugonvi kila kukicha kwa kweli hii siyo staha ni karaha.
Nimeshuhudia ndoa nyingi zilizoingiwa mpasuko, 10% zimenusurika na kurudia hali ya uelewano, another 10% wametengana, ila 80% wapo pamoja lakini hiyo songombingo ndani ya nyumba ni hatari tupu. Ugumu wa suruhisho ni akina wake.
Wamekataa kutafuta suruhu, na imekuwa kama zimwi likujualo halikuli likakwisha. Kwa kweli nawapa pole hao waliopo kwenye mahusiano ya hali hii. Wanaoumia zaidi ni watoto.
Nyumba ni mahala ambapo
-baba anahitaji apate pumziko baada ya harakati za siku nzima,
-baba ajisikie anapa-miss pindi awapo nje ya nyumba.
-ni mahala pakusanyiko la familia, pawe patulivu na upendo.
Ushauri wa buree kwa wanawake na akina dada, wababa wanahitaji kupendwa, na kubembelezwa. Wapeni raha badala ya karaha.
Nawatakia mdumishe upendo wa AGAPE daima milele.