Mkuu,mwambie mkeo kuhusu kero hiyo,ni ukwel hili suala lipo nam ni mhanga,unarudi kutoka kwenye majukumu ya kimaisha,unakuta vyombo havijaoshwa,sebule chafu,nguo nazo chafu,yeye mwenyewe mchafu,hadi shuka umwambie abadilishe au azifue,na anachokifanya hakionekani,tangu asubuhi alivyoamka alichokifanya hakionekani,nikagundua ni uvivu,na mimi napenda sana shuka nyeupe,nakumbuka siku za kwanza kwanza aliniulizia,kwanini? napenda shuka nyeupe,nikamjibu hazifichi uchafu na zinamlazimisha Mtu awe msafi hata kama hataki,kwa hiyo nilipogundua ni mvivu nikawa namsema kiutani lakini ujumbe unafika,wakati mwingine nilikuwa nafanya kwa vitendo kumuonesha nami nnaweza,hadi akabadilika mpaka sasa ni msafi,hivyo ni vizur kumsema,sababu ni nadra kwenye ndoa wote kuwa wasafi,lazima mmoja atakuwa mchafu,hivyo yule msafi atamrekebisha mwenzake,wa kiume au wa kike,hivyo mkuu nakushauri chukua nafas yako mapema,kabla mambo hayajaharibika.