Wanavyuo wasilazimishe kujiunga na chama fulani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanavyuo wasilazimishe kujiunga na chama fulani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, May 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  VYAMA vya siasa nchini vimeshauriwa viwaachie uhuru wanafunzi wa vyuo vikuu wachague vyama wanavyovitaka kwa utashi wao na si kwa kulazimishwa.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Mtera kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Lameck alipokuwa akizindua tawi la chama hicho katika Chuo cha Biashara (CBE) mjini Dodoma.

  Alisema, wanasiasa hawana budi kuwaacha wasomi wa vyuo vikuu kufanya uamuzi binafsi na kuchagua chama wanachokitaka kwa utashi wao bila kulazimishwa.

  Lameck alisema, kwa kuwa wanavyuo ni watu wazima na wasomi ambao wanaweza kufanya maamuzi yao bila kusimamiwa na mtu kwa manufaa ya taifa lao hakuna haja yakuwachagulia kitu.

  “Suala la wanasiasa kufanya shughuli zao katika vyuo ni kitu ambacho hakiruhusiwi na sidhani kama tunatakiwa kufika huko… lakini kama wanataka tufanye hivyo basi iwe hivyo,” alisema Lameck.

  Aidha aliwataka wanavyuo kuacha ushabiki wa vyama bali wafanye kitu chenye manufaa na taifa lao.

  “Vijana wanatakiwa kuangalia tumetoka wapi tupo wapi na tunakwenda wapi ili tuweze kulijenga taifa hili katika misingi imara kiuchumi na si kufanya mambo yetu kisiasa zaidi,” alisema.

  Aliwashauri vijana hao kuwa makini katika kuchagua chama ambacho wanaona kuwa kina manufaa kwao na taifa kwa ujumla na pia chenye msingi thabiti katika kutekeleza ilani yake.
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Maoni yake ni sahihi kwa upande mkubwa tu.
  Siasa za mavyuoni zinatakiwa zichukuliwe kwa uzito mkubwa sana. Sababu mavyuoni ndipo kwenye azina kubwa sana ya mustakabali wa nchi yoyote duniani.
   
Loading...