ndugu PLATO nakupongeza kwa thread yako, huo ni mtazamo wako. Members 8 wa kwanza kujibu thread yako wameanza kwa mishangao, nahisi hawakutarajia kukuta walichokikuta, mimi binafsi nakubaliana na wewe lakini pia naweza nikawatetea wanachuo hao kama ifuatavyo;
1; wanafunzi wengi kwa sasa wanatokea shule za kata au hata kama ni shule kongwe za serikali mf. galanos, tosamaganga, old moshi,
pugu.....etc, hazina walimu ambao wengi wao kwa sasa wanakimbilia private school kwenye malipo makubwa, au hawafundishi kwa
ufanisi coz wana part time kwenye shule za kulipia, mwanafunzi huyu akiwa chuo hawezi kuwa na critical thinking coz msingi wake ni
madesa (handout) wanazonunua wakiwa sec. ili wakariri waweze kufaulu.
2; wakiwa chuoni wanabaguliwa kimadaraja, yaani means test, anaepewa 100% hawezi kuwa sawa na wa 40%, huyu wa 40% akipewa
bumu analigawa kulipa sehemu ya ada ya chuo, (pata picha maisha atakayoishi akiwa chuo km udsm na anaishi mabibo, na
anatoka familia ya akina kajamba nani km mimi, wkt huo ana wadogo zake wapo shule za kata wamekosa ada ya elfu
20 inabidi awalipie, bado hujajumuisha na bei za vitu kuwa juu) WALAHI HATAKWEPA DESSA.
3; System ya vyuo kuingiliwa na mashushu wanafunzi au wahadhiri (siwezi kuthibitisha hilo) huwafanya wanachuo kuishi kwa hofu na
hivyo kuwashawishi kuandamana hasa kwa chuo cha mkuu wangu MKANDALA km ilivyokuwa kwa mkuu wangu wa ukweli
PROF. LUHANGA is impossible.
my take, ni kwamba huyu mwanafunzi aliyelegea kwa njaa, anayeingia library kudesa hawezi kujenga hoja na hawezi kuandamana coz hapo alipo anafikiria akam'bomu nani amsaidie hela ya kauzu maana kafeteria hapaingiliki na mda huo kachoka kutembea kwa miguu kutoka mlimani hadi mabibo jua kali, NA TUMSAIDIE MWANAFUNZI HUYU KWA KUUNG'OA UTAWALA WA KIBAGUZI ILI ASOME KWA KUJIAMINI TOFAUTI NA SASA, TUSIMLAUMU TU. hilo la kondom kuzagaa inawezekana ni kwa wale wachache wanaotoka familia bora maana huyu maskini sidhani km ananguvu ya KUJIGIJIGI wkt hajala chakula cha maana japo akifanya hivyo si mbaya maana anajaribu kusahau shida zake. KUMBUKA chuo wapo wanachuo wakike pia hawana hela hivyo wanajamii kutoka posta kazini au kinondoni huchangamkia hizo tenda za wasomi wakike wanaoganga njaa ili shule iishe wapate wao mradi, so huenda humalizia shida zao hapo hapo maeneo ya public area ili watoto wa watu wawahi discussion na wenzao.