GedsellianTz
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 1,348
- 1,803
Wanaume wengi ambao hujifanya wajinga huwa waerevu daima na wanaume wengi ambao hujifanya wajanja huwa wajinga daima,sababu kuna ukubwa wa mwili na udogo wa akili ,harafu kuna udogo wa mwili na ukubwa wa akili .Mwanaume mjinga machoni pa wanaume wajanja ni yule anayewahi nyumbani kukaa na familia yake ,kucheza na watoto wake na kufanya home work na watoto wake ,na kumsaidia mke wake kazi za nyumbani.
Mwanaume mjinga aingiapo ndani hata mtoto akiwa ananyonya ziwa la mama yake asikiapo sauti ya baba yake huliacha ziwa la mama yake na kumkimbilia baba yake ,sababu baba yake ndio hazina ya furaha na faraja .Kuna wanaume bora ambao hujinyima furaha yao na kuikimbia starehe na kuipa familia kipaumbele kwa kila jambo,mke wake mwanaume mjinga humfanya mke wake muhasibu wake na rafiki wake wa karibu ili kutengeneza familia yenye upendo na mshikamano.
Daima palipo na mwanaume mjinga ambaye ni mwerevu nyuma yake huwa kuna mwanamke bora mvumilivu mwenye upendo na faraja kwa mume wake,wanawake bora wenye mapenzi ya dhati na waaminifu wapo wengi ila hawaonekani kama wanawake wazuri wasio na sifa za kuwa mama bora na wake bora,wanaume bora wamejaa kila kona wakihaha kutafuta wanawake bora na waerevu.
Utamu wa ndoa ni kuwa na mwanamke mnyenyekevu na muadilifu na kuwa na mwanaume mjinga , mwerevu na msikivu kwa mkewe .Daima mtoto huwa na afya ya mwili na afya ya ubongo kwa tabasamu la baba yake na kicheko cha afya cha mama yake.It is easier for a father to have children than for children to have a real father.