Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,312
- 8,754
Naskia Mlio wa Simu yangu Ndogo ya Mkononi aina ya Nokia ya Tochi, ilikuwa ni saa kumi na mbili Jioni kasoro dakika kumi na tatu siku ya Jumatano wiki iliyopita Nikiwa natoka Mitaa ya Msasani Pale Kinondoni..
Rafiki yangu toka Mbulu ananipigia simu ananieleza kwa sauti iliyojaa simanzi ya kweli,sauti yenye hofu ndani yake taratibu kwa masikitiko akanieleza kwamba Mtu Mmoja Mwanamume ninayemfahamu (Binti yake tuliwahi Kupendana), Amejinyonga na kufariki. (Apumzike kwa Amani)
Nikamuuliza kwa Undani Sababu ya tukio hilo ni nini? Jibu Nililopata ni MGOGORO WA NDANI YA NYUMBA, Yaani Mgogoro wa Mke na Mume, Hapa tunajua Mgogoro ambao hasa unaweza kupelekea Mwanaume Kujinyonga ni USALITI, Kusalitiwa na Mke..
Turudi Nyuma, Jarida Moja la Nchini Marekani lilitoa takwimu kwamba Mapenzi ni Chanzo cha kwanza kinachoongoza kwa Watu Kujiua, Pia isitoshe Wanaume Ndio Tunaongoza katika kesi hii.. ya Kujinyonga.
Kama Mnakumbuka Nafikiri Mwaka Huu Mwanzoni Mwanafunzi Mmoja wa kiume alikuwa anasoma CBE Campus ya Mbeya kama sikosei alijitupa Kutoka Ghorofani baada ya kugundua Mpenzi wake anamsaliti..Alifariki (Apumzike kwa Amani)
Mfano Hai Mwingine Mwanzoni Mwa Mwaka 2006 Nikiwa Mwanafunzi Shule ya Sekondari Ufundi Moshi Nilitokea Kufahamiana na Mshikaji Mmoja Mtaratibu sana akawa kama Bro wangu wa Shule , Nilikuwa Kidato cha Kwanza Yeye alikuwa Kidato cha Sita, Alifanikiwa kufaulu na Kujiunga Masomo yake ya Elimu ya Juu.. Hatimaye akafanikiwa Kuwa Mhandisi wa Umeme.. Huyu Bwana Alioa, Mke wake alikuwa Mhandisi wa Maji Pale Mjini Mbeya, Walikuja Kupata tatizo la Ndani ya Nyumba yaani Mgogoro Mwishoni mwa Mwaka Jana..inasemekana Mke wake alikuwa akitoka na Mhandisi Mwenzake ofisini waziwazi.. Jamaa alimuasa bila Mafanikio.. akachukua uamuzi wa kujiua kwa kubwia dawaa.. Alifariki Dunia, Alikuwa mtu Mmoja Mstaarabu saana (Apumzike kwa Amani).
KWANINI WANAUME HUJINYONGA KWA SABABU YA MAPENZI?
Biblia Takatifu Kupitia 1Petro 3:7 inatuambia Kwamba
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
Yaani tukae na Wake zetu kwa akili ( Sitaki kutafsiri ila kwa utashi wa Fikra zako Jaribu kuutafakari Mstari Huu)
Wanaume Wengi Kama Kuna Hatuwezi Kusamehe ni USALITI, Ngumu Mno.. Mwanaume kusamehe Hicho Kitu, tuachane na Hilo..
kwanini mtu unajinyonga kwa sababu ya Mapenzi? Sababu kubwa inaanzia Pale unapompa Mke/Mpenzi Moyo wako wotee.. Halafu afanye tofauti na ulivyotegemea, akuache/akusaliti (SIPOTOSHI).
Kitendo cha sisi wanaume kutokutaka kudhalilika kwa sababu ya USALITI wa wake/wapenzi wetu.. yaani kutokueleza kwa mtu ili angalau yale maumivu yatoke, wanaume ni ngumu kufanya hivi (Wazee Husema Kuchapiwa ni Siri ya Ndani, imegharimu Maisha ya Wengi).. atakufa na siri labda watu wajue wenyewe (Hapa stress huongezeka).
WANAUME USHAURI HUU HAPA.
Biblia takatifu Kupitia 1Petro 3:7

Ndugu zangu WanaJF Kitaaluma tunasema Kujinyonga ni (Short term solution for Long term Problem) Yaani SULUHISHO LA MUDA MUPI KWA TATIZO LA MUDA MREFU. Kwa Maana ukifa wao wataendelea kufurahia Maisha..
Pia ndugu zangu tujiulize kwanini kwa Wazee wetu haya matukio ya Kujinyonga kwa sababu ya Mapenzi hayakuwepo kama ilivyo sasa? Ni kwa sababu hawakuwa na Mwanamke Mmoja.. Hawakuwa wakipata stress kwa maana ikitokea Mmoja akisumbua wengine wapo. Hawakuwapa Nyoyo zao wanawake wao kizembe kama vijana wa sasa walivyo na Ndoa zao Zilidumu..
Isitoshe katika ulimwengu wa sasa Uliojaa Usaliti (Kumbuka Mwanamke anashawishika Kirahisi, Ndio Maana hata Biblia inatuambia Eva alishawishiwa na Nyoka ili alionje lile tunda la Mti wa Katikati Akamwangamiza na Adam Pia kwa Kumuonjesha lile Tunda, Nyoka alijua Mwanamke ana Tamaa, na mtu mwenye tamaa ni rahisi sana kumshawishi, Eva akashawishika)..Mwanaume Mwenzangu Narudia Usimpe Mwanamke yeyote Moyo wako, Kazi ya Moyo acha iwe Kusukuma Damu.. la sivyo utajutia.
Kwa Kuhitimisha mara litokeapo tatizo linalokupa Msongo wa Mawazo usiache ukae nalo Moyoni, wataarifu ndugu jamaa na marafiki pia wataalamu ili tatizo lako liweze kushughulikiwa!
Mwisho Tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu Ndugu zetu, Jamaa Zetu na Rafiki zetu waliotangulia Mbele ya Haki Kwa Kujinyonga Labda kwa Sababu ya Kutokujua..
Mwenyezi Mungu Awapumzishe kwa Amani na Awape Raha ya Milele!,
Tunaomba haya kwa Njia ya Bwana wetu yesu Kristu Mwanawe, Anayeishi na Kutawala nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu Mungu Daima na Milele!. Amina.!
Mimi
Architectus