Wanaume wengine hawajielewi kabisa aosee

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,840
⚠️😳 Kwa mshtuko na masikitiko ya kutoamini Jamaa huyo kwa jina la Chido amejitosa waziwazi kuomba ushauri mtandaoni kufuatia ndoa yake ya miezi mitatu tu kupumulia mashine kwasasa

Chido amesema alimsaliti mke wake kwa kuchepuka na mdada flani na kwa bahati mbaya au nzuri mke wake akajua na kwa ushahidi wote, baada ya mke kujua akaanza kumpuuza mazima mumewe huyo mithili ya mzoga.

Chido amesema alijua atasamehewa tu na mke wake lakini kilichofuatia Chido amesema mke wake kwasasa na yeye anamringishia na aliyekuwa boyfriend wake wa kipindi hivho hali ambayo Chido amesema inamuumiza sana kama mume kwani hakutegemea mkewe angechukua hatua hiyo mapema sana

Amesema baada ya hapo ikanidi amuangukie mkewe kumuomba msamaha huku anaangua kilio lakini bado hajasamehewa na mke wake

Hiyo tisa, kumi mkewe kwasasa amemuambia hahitaji tena kuendelea na hiyo ndoa hivyo aoe mwanamke mwingine na pia amesema familia yote ya mke wake ipo upande wa ndugu yao hakuna anayemuunga mkono yeye mume kwa usaliti aliomfanyia mkewe katika ndoa ya miezi mitatu tu hivyo.Chido hajui afanye nini kuinusuru ndoa yake

Chido alipoulizwa na na mmoja wa waliotoa maoni katika post yake sababu ya kumsaliti mkewe wakati ndoa yao ni mbichi, amesema alichepuka bahati mbaya kwa kuteleza na aliona ni jambo la kawaida kwa mwanume kuchepuka na hakutarajia mkewe angekaza kamba kiasi hicho

Mtoto maoni mwingine alipomwambia labda ajaribu tu kumuomba tena mkewe msamaha anaweza samehewa, Chido nae amesema alishamuomba msamaha mkewe mwanzo kwahiyo hawezi tena kuomba msamaha mara ya pili huku akionekana kuumia zaidi kwa kusema kwanini mkewe amringishie na aliyekuwa ex boyfriend wake
 

Attachments

  • FB_IMG_1689408890970.jpg
    FB_IMG_1689408890970.jpg
    41.4 KB · Views: 8
nitoe rai na TAHADHARI kwa ndugu, jamaa na marafiki zangu wa kiume,..siku nikikubaini kuwa ww ni kopo, bwege kama huyu jamaa, unaemuangia mwanamke na kulia tena kwa machozi,..na kupandwa kichwani na ukaja kwangu kuniomba msaada wa ushauri,...uta ambulia manundu na kuvunjwa mguu....#pumbavu.... he's not man enough
 
Back
Top Bottom