kichakaa man
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 5,487
- 5,111
Imekuwa ni jambo la kawaida ukiwa kijiweni au popote pale palipo na mkusanyiko au story za kiume ni Mara nyingi utasikia kila mwanaume yeye ni bingwa wa mapenzi na ana maumbile makubwa ya kiume, anafanya mapenzi kwa Masaa mengi, anamfikisha mwanamke kileleni na kila aina ya ufundi wa kitandani yeye anaujua kwahiyo mwanamke hawez kumchoka na kumchukia lakin pamoja na majigambo na kutafuta sifa wanaume hawa wamekuwa ni ovyo kabisa kwenye mahusiano yao kwani wameshindwa kujenga mazingira rafiki na misingi bora na imara kwenye mahusiano yao hivyo kujikuta wanaharibu zaid na zaidi kwa tabia zao za kutokupenda maelewano na kuwapatia nafasi wake/wapenzi kuweza kufanya maamuz au kuheshimu maamuz ya wapenzi wao na hivyo mwisho wa siku wanaharibu upendo na furaha na matumaini ya familia kwa tabia za ukorofi na ubabe usio na faida
Lakin upande wa pili wanawake hawa kiukwel wamepoteza tumaini kwa tabia za waume zao kutokuwajali wala kuwasikiliza au kuheshimu mawazo yao hivyo kujikuta muda wote ni wenye huzuni,masikitiko na ni watu waliokata tamaa na maisha , wamekosa tumaini la maisha . japo wengi wameendelea kuwa wavumilivu juu ya manyanyaso na kuishi maisha ya uoga na mateso ya hawa wanaume zao , na wengine kwa kukosa uvumilivu wameamua kuchepuka ili kutafuta faraja na kujiepusha na manyanyaso kutoka waume zao wenye ubabe usio na faida.
Matukio nayafananisha na maisha ya Watanzania wa sasa jinsi ambavyo wengi wao wamejaa majonzi ,huzuni na kukataa tamaa kwa sababu ya aina ya utawala wa awamu hii ambao umekuwa na tabia ya kutokujali misingi ya sheria na utu wa raia wake , aina ya viongoz ambao wameamua kuwa miungu watu kwa kutokukubal kukosolewa pale wanapo kosea , wanavunja katiba ya nchi mchana kweupe bila aibu na hawana uoga ,
Viongoz ambao kipindi cha shida wameamua kukaa mbali na wananchi wao hasa kiongoz mkuu wa familia hii .mifano ipo mingi tetemeko la kagera, janga la njaa , tukio la kushindwa hata kuhudhuria msiba Mkubwa wa Taifa kwa kupoteza watoto 30 lakin kiongoz mkuu kaishia tu kutuma barua ya pole , je ameshindwa nin kuhudhuria tukio la kuweza kuwafariji wananchi wake wajione wanapendwa na mkuu wa familia
Maamuz yenye kujenga chuki na upendeleo , wananchi wengi wanalia na maamuz yenye kuwatia u masikin na simanzi , mfano kinachoendelea sasa kuhusu vyeti feki watumishi kutimuliwa huku yule kijana kutoka kijiji cha call me J akiendelea na nafas yake ya kuwa kiranja wa mkoa wa bandari salama au kwa mzizima wenye wanaitaga bongo. Ni moja kati ya vitu vinavyoumiza sana
Wananchi wanakata tamaa kuona mahakama inaingiliwa kufanya maamuz mfano mdogo uwepo wa kaimu jaji mkuu na mikasa mingine ya kuelekeza nin mahakama ifanye bila kufuata sheria inasemaje , upande wa pili bunge limekuwa halina nguvu tena kusimamia hii familia maana mkuu wa familia anawapangia nin cha kufanya
Watanzania hawa wanaona uonevu had kwa viongoz wa hii familia mfano yule katibu mwenez na aliyekuwa waziri wa michezo bila uoga walimtolea manati ya mzungu mbele ya vyombo vya habari ili tu kumzuia asitoe ya moyoni
Mkuu wa familia anawachukia zaid watoto zake wanaofanya biashara na kuwaona ni wapiga dili na hawastahili kupewa nafas ya kufanya biashara zao katika mazingira rafiki lakin bado mkuu wa familia bila huruma wala aibu amewapiga roba ya mbao watumishi wake wanaomsadia kaz za shambani kwa kuwasimishia mishahara, anawatumbua bila kujali unatakiwa kustaafu lin, amegoma kuwapandishia mishahara na hatak kutoa ajira tena ila acha kabisa ana mtoto wake mmoja alifeli kwa kupata sifuri kabisa yaani ni full FFFFFFFFFF lakin ndiye anapendwa kwa sababu ya tabia yake ya kuropoka vitu bila ushahid na ukorofi wake
Mkuu familia pamoja amekuwa hapendi kupewa ushauri wa ukwel na ukimwambia ukweli hata kama huna jipu utatumbuliwa tu maana yeye ahadi yake ni kuona watoto wanaishi kama mashetani .
Kuna mambo mengi yanatia huzuni lakin naomba niondoke hapa maana namuona mtoto wa wake yule Mwenye ufaulu wa F yupo na wenzie hapa wameshika zile manati za mzungu huyu Mr FFF naona analalamika hapa usiku huu wa saa 4 usiku anaenda kuchukua flash kwenye kituo cha TV cha mawingu . najaribu kujiuliza hiyo flash ina nin had anaenda na mitutu kudai . jamaan mtanijuza nin kinaendelea huko anakoenda kudai hiyo flash .
Yapo mengi sana , ndani ya hii familia ya watanzania bahati nzuri Leo nimepita nje ya nyumba ya hii familia ni wana huzuni Mara mbili kwa kupoteza watoto wadogo taifa la kesho kwa mkasa mbaya wa ajali .naomba mungu awape nguvu na kuwapumzisha hawa watoto mikonon mwa mwenyezi mungu
Nawakumbusha tu hawa watu wakiona mateso yamezidi ipo siku wataitafuta haki kwa nguvu