Wanaume wawili wakubaliana kuoa mwanamke mmoja

Wanaume wawili wakubaliana kuoa mwanamke mmoja

kila mfumo una hasara zake demokrasia haiko perfect. ukiacha demokrasia mifumo mingine ndio haifai kabisa.
kwa nchi zetu demokrasia bado sana kufanya kazi perfect coz viongozi wanatanguliza maslahi binafsi mbele then fuatilia vizuri nchi zote zenye demokrasia imara zilianza kutumia hiyo demokrasia baada ya kuwa na maendeleo,
 
Jamani mbona mnashangaa sana? Mbona hapa TZ ilishatokea kitambo kule jimboni kwa Mizengo Pinda? Hata humu iliwahi kubandikwa. tofauti ni kwamba wa TZ hawakuwekeana mkataba
 
Huyu mama atakua ana kitu tamu sana,haiwezekani wanaume wakamng'ang'ania hivo
 
lord have mercy on this world!! mmoja tu niliyenaye akiniamulia mapafu hu-stop kupumua, itakuwa marijali wawili ndani!?? awaonee huruma wenzie, kuna wenzie kutwa kurogana hawana hata wa kuwadanganya, ye wote wake. hubby Asprin r u ready nikumix na mtu??
 
Last edited by a moderator:
Wanaume wawili wa Kenya, Sylvester Mwendwa na Elijah Kimani wamekubaliana kumuoa mwanamke mmoja baada ya kubainika kuwa kila mmoja alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi na hakuna aliyekuwa tayari kumwacha. Wanaume hao wakazi wa Kisimani Kisauni, Mombasa walikubaliana kwa mkataba maalumu wa maandishi juzi, wakisema kwamba wako tayari kushirikiana kinyumba na mwanamke huyo na kumaliza ugomvi baina yao.

Walichukua uamuzi huo baada ya kubaini kwamba kwa pamoja wamekuwa na uhusiano na mwanamke huyo mjane, mama wa pacha kwa zaidi ya miaka minne bila ya kugundua. Walibaini ukweli huo baada ya fumanizi lililozuia ugomvi baina yao. Hata baada ya mwanamke huyo, Joyce Wambui kuambiwa achague mmoja kati ya wanaume hao ambaye angeishi naye alisema hawezi kuishi bila mmoja kati yao.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Usalama, chini ya Mpango wa Ushirikiano baina ya Polisi na Raia, Abdallah Abdulrahman, Mwendwa na Kimani waliamua kuishi na Wambui baada ya kushindwa kuelewana ni nani kati yao anayestahili kuwa mumewe kwa sababu wote wanampenda naye anawapenda wote wawili. "Kila mmoja alisema asingeweza kuishi bila mwanamke huyo ambaye ni mjane, ndipo wakaamua kuandikiana mkataba kuhusu namna ya kuishi na mwanamke huyo," alisema.

Mkataba wa ndoa

Abdulrahman alisema uamuzi huo ulifikiwa ili kusuluhisha mzozo huo. Alisema mkataba waliotia saini unaeleza kuwa mmoja wa wanaume hao atakuwa na wakati wake wa kumtembelea mwanamke huyo. Mkataba huo pia unasema kuwa wataishi kwa kuheshimiana na hakuna yeyote kati yao atakayechukua zamu ya mwenzake kumtembelea Wambui. "Nilijaribu kwa kadri ya uwezo wangu kuwapatanisha lakini hakuna aliyetaka kumwachia mwenzake mwanamke huyo. Niliposhindwa niliwaacha nikarudi ofisini," alisema Abdulrahman.

Alisema alishangaa wanaume hao walipofika ofisini mwake baadaye na kutia saini mkataba ambao walikubaliana kuishi na mwanamke huyo kwa zamu. Mwendwa alisema Wambui akijifungua mtoto atakuwa wao wote kwa sababu itakuwa vigumu kujua baba yake isipokuwa kama watafanya uchunguzi wa vinasaba, DNA. Alisema wote wawili wanasimamia malipo ya kodi ya nyumba, chakula na matumizi mengine ya Wambui na watoto wake pacha.

Lakini mpango huo umepingwa vikali na wakazi wa eneo hilo wakisema ni kinyume na utamaduni wa Kiafrika na maandiko ya Biblia na Quran. "Hawa watu wanafaa kushtakiwa kwa kuvunja sheria ya ndoa katika Katiba, huu ni unyama," alisema mkazi wa Kisauni, Tumaini Juma.

Wakubaliana kuoa mwanamke mmoja - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Source
Two Men Agree to Marry Same Woman - YouTube

Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda kwa kusaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.


Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao. Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.


Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.


Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.


Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.


Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.


Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angefunga nao ndoa bila ya wao kujuana.


Lakini walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi kwa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao, alishindwa. Akasema anawapenda wote wawili.


Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda kumjulia hali.'


Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.


Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
 
Ina maana hawaoneani wivu? Hiyo miaka minne si alikuwa anaficha!! Sasa iko wazi wangemwacha tu maana sio mwaminifu huyo!! Akitokea mwingine akampenda si ataanza uhusiano naye!!! Huyu mwanamke ana tatizo. Mwanaume tu kuwa na wake zaidi ya mmoja ni noma sasa mwanamke je ni kitu cha kawaida hicho? Hiki si kitu cha kawaida kabisa. The woman must be possessed!

Mkuu si unajua sasa hivi mambo ya usawa wa kijinsia they also need to possess! mfano hai ndo huu!
By theway hata hapa Tanzania kuna baadhi ya makabila huko kusini na somewhere Mororgoro wale wanao practice Matrimonial system they do also possess! fatilia mkuu pia somehwere uhindini!
 
afadhali hao,mie nilishangaa kipindi cha mimi na tanzania mama analala na mwanae.....mnh:embarrassed1:
 
lord have mercy on this world!! mmoja tu niliyenaye akiniamulia mapafu hu-stop kupumua, itakuwa marijali wawili ndani!?? awaonee huruma wenzie, kuna wenzie kutwa kurogana hawana hata wa kuwadanganya, ye wote wake. hubby Asprin r u ready nikumix na mtu??
Labda kama huyo mtu atakubali kuwa mke mwenza. Mke wa ujana wangu unataka nibemende mashoga??
 
Two men on Sunday agreed to share a woman in a written contract in which they vowed never to fight over her. The pair from Kisimani in Kisauni, Mombasa County, made the deal after realizing they have both been having an affair with the woman for more than four years.#polyandry
When asked to make a choice, the woman also declined, saying she could not live without either of the men. This made them agree to take turns to live with her.
Mr Sylvester Mwendwa, one of the ‘husbands’, said they decided to share the woman with Mr Elijah Kimani.

source:Love rivals sign contract to share one woman

Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, shangaa ya Kenya ambako hawajawa na ndoa Bongo wanaume wawili wanashare mwanamke mmoja kwa ndoa halali za kiserilaki, upo hapo?
 
Back
Top Bottom