Wanaume wanataka kukirimiwa

Wanaume wanataka kukirimiwa

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Helooooz mabestito

Natumai mnaendelea vyema wapendwa wangu.
Mama mfundajji ndo nimeingia mzima mzima tena leo naona somo la juzi wengi wenu hamkulielewa sasa leo nimekuja somo MARIDHAWA kwa wanawake wenzangu ambao wako
katika mahusiano ya NDOA na wale ambao mnajiandaa kuingia kwenye mahusiano pia


Kuna mambo ya msingi ambayo mwanaume yeyote huhitaji kupata kutoka kwa mke wake mpenzi AU kwa rafiki yake kipenzi na kinachotakiwa kwa mwanamke ni yeye kufahamu nini mwanaume anahitaji na kuwekeza kidogokidogo kwa kuongeza jitihada na muda ili haya mahitaji kuwa kitu halisi kwa mwandani wake. Mama MFUNDAJI nimeigia vyema leo sitaki kuwarusha roho kama juzi
mpaka hamkuelewa undani wa somo lile mnisamehe wale ambao hamkupata radha ya somo la juzi.

Je ni Vitu gani mwanaume huhitaji sana kutoka kwa mke wake au mwenzi wake?
Wanawake ni viumbe tofauti, wao ni walezi kwa asili, waumbaji wa vitu, wasimamizi wazuri na wabunifu sana. Wanaweza kwa urahisi sana kuelezea kitu kilichopo kwenye akili zao likija suala la ishu yoyote ya biashara kama kununua au kuuza.

Wanaweza sana kwenye mambo ya design na hata mawasiliano.
Ila likija suala mwanaume hapo ndiyo kuna tofauti. wanakuwa hawajua nini wanaume wanapenda juu yao au kutoka kwao wanabaki wako wameduwaa wanaona wanaume wanawanyanyapaa kumbe sivyo hatujatambua kiundani kitu gani wanaume wanapenda kutoka kwetu tuwatendee au TUWAKIRIMIE

MAMBO YA MSINGI MATATU AMBAYO WANAUME WANAPENDA KUONA TUMEWAFANYIA WAO

A: Wanaume huhitaji mwanamke anayejua kukubaliana/kuafikiana

1. Je kama mume wako anapenda kuangalia au kucheza soccer siku za weekend kwa ajili ya kujiliwaza huwezi kuwa naye?

Kuna ubaya gani wewe kushangilia kile mume wako anapenda (hobbies)
Kumbuka maisha ndivyo yalivyo msipofurahi pamoja na kuwa na fun pamoja usitegemee siku mambo yabadilike yenyewe tu kuna kitu unahitaji kufanya sasa ili kesho iwezekane.

2. Penda kufanya pamoja kile kitu mume wako anakipenda katika maisha inaweza kuwa ni mpira, kimba au kwenda kutembea sehemu yoyote ili pamoja au matamasha na michezo mbalimbali.
Kumbuka unaweza kuwa wewe hupendi kwenda naye huko yeye anapenda kwenda, lakini kuna wanawake wanafurahi kuwa naye huko wewe umekataa kwenda na hana njia kwani ni kitu anakipenda na ni sehemu ya maisha yake (kama hatendi dhambi).

B: Wanaume wanahitaji mwanamke anayejua mambo
1.Huwezi kutenganisha habari za siasa, michezo, biashara, sayansi na mambo ya kimataifa na mwanaume, hivyo usijiweke nyuma sana unahitaji kuwa mtu wa karibu kupiga naye story za mambo kama hayo, jitahidi na wewe kuwa wamo sio wa kuja jana toka mkoa fulani hiv
Inawezekana jioni kabla ya kulala mkawa na glass ya juice mnakunywa wawili huku watoto wamelala, wewe mwanamke kwa ujasiri shusha story za michezo mambo ya Chelsea, jamani chelsea ni timu yangu acha niitaje au hata Yanga na Simba just for fun, au hata habari za mfalme Daudi au business ambazo umezitafiti hapo mwanaume atajua nina mke ndani ya nyumba.
2. Wapo wanawake mume akianza kuongea habari za siasa, michezo au business anaondoka zake na kumwacha naamini wanaume hapo huwa hawafurahii kabisa. Nakwambia ukijua kuongea na mumeo mambo ambayo wanaume wote wanayapenda utafahamu mambo mengi sana kuhusu ulimwengu, watu na ninyi wenyewe.

C: Wanaume wanapenda wanawake ambao wanajishughulisha na kuwajali wao zaidi/ kuchangia majukumu ya familia kwa ujumla

Huwa kuna kawaida kwamba mwanaume katika jamii zetu za kiafrika ndiyo anakuwa mwamuzi wa mambo mengi kiasi kwamba hata wanawake wenyewe hutambiana kwamba jana mume wangu alinipeleka dinner sehemu.

Je, itakuwaje kama na wewe mwanamke siku ukamwambia mume wako leo pamoja na watoto tunaenda lunch sehemu au dinner sehemu kula, pamoja na watoto wenu kwa hela yako au bajeti yako au maamuzi yako. Wakati huo huo umetinga kiwalo chako cha nguvu (sexy) hadi unamkumbushia zile enzi zenu ambazo zilifanya avutiwe na wewe hadi kukuoa.

1 Wanaume wanahitaji wanawake wa aina hiyo ambao siku zingine wanafanya vitu romantic au sexy angalau hata kwa mwaka mara moja siyo mwaka mzima hujafanya jambo lolote la kuimarisha mapenzi. Wanaume wanahitaji mwenzi siyo mtu wa kuishi naye chumba kimoja
Kuagana asubuhi na kuja kukutana jioni bila kuongea chochote mchana mzima ni dalili ya uhusiano usio na afya kabisa.

Jaribu kufikiri mwenyewe hivi ukiondoka asubuhi unawasiliana na mumeo mara ngapi?
Siku hizi karibu kila mtu ana simu ya mkononi, unaweza kutuma sms, au kumpigia just to say hi honey! Mbona wakati wachumba sms zilikuwa zinatumwa hadi vidole vikaota sugu, leo kunani?
Hamu na msukumo alionao mmoja kwa mwenzake ni msingi wa kuonesha afya na mahusuano yenye furaha.

2. Wakati mwingine mahusiano huenda bila mawasiliana ya mara kwa mara lakini hiyo ni sumu kubwa sana kwani inaweza kufikia kipindi hakuna hata kutakana, hamu ya kila mtu kwa mwenzake hupotea na hapo ndipo watu sasa huanza kuishi kama vile watu tofauti walioamua kuishi nyumba moja na chumba kimoja lakini ule moto umetoweka.

NAWAFUNDA JAMANI TUKAE SAWA KWANI TUMEJISAHAU KATIKA NAFASI ZETU

Kwa hiyo kama wewe ni mwanamke hakikisha unakuwepo katika mahusiano kwa maana kwamba unahitaji kumtia moyo mumeo, kumuinua pale anapokata tamaa uliza nini kinaendelea asubuhi, mchana, jioni na usiku, pia akifanya kitu kizuri mpe sifa na hongera.

Jifunze kwa busara na hekima kujua nini kinaendelea katika maisha ya mume wako na pia onesha kwamba unamjali sana (care) na kwa njia hiyo automatically atakupenda zaidi na ndoa yenu itakuwa imara zadi. Ama mahusiano yenu yatakuwa bora zaidi na mtakuwa kila mkipita watu wataiga mfano wa ndoa au chumba zenu

Naashia hapa next week nitaleta SOMO lingine hili sasa litawahusu wanaume kwetu pia

Wasalaam;

Ladyf
 
Imenena, itasaidia hata wanawake wengine kukumbuka ni nini na nini wasiache kufanya katika maisha yao na wenzi wao.
 
1468068354703.jpg
 
Back
Top Bottom