WAnaume wa rombo waamua kufanya unyama

WAnaume wa rombo waamua kufanya unyama

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2013
Posts
1,301
Reaction score
743
Mkuu wa wilaya Rombo Bi Agness Hokororo ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kuwakamatwa wazazi na walezi ambao hawatatoa ushirikiano kwa polisi katika kesi za watoto wao kubakwa na kulawitiwa ili wachukuliwe hatua za kisheria kuanzia sasa.
Bi Hokororo ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo kikuu cha polisi wilayani Rombo na kukuta mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka miwili na nusu amebakwa na kijana mmoja ambaye hajakamatwa.
Amesema, vitendo kama hivyo vinashamiri katika jamii na wazazi wamekuwa wakitumia mila potofu za majani aina ya masale kuombeana msamaha na pombe ya kienyeji aina ya mbege na kusababisha kesi hizo kufutwa kwa kukosa ushahidi huku watoto wakike wakiathirika zaidi.
Mkuu huyo wa wilaya ya Rombo ametoa mfano kuanzia mwezi juni mwaka huu ambapo wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wamebakwa na kusababisha mimba 24 na katika wiki moja iliyopita vijana watano wanashikiliwa na polisi kwa kulawiti watoto kati ya miaka miwili hadi saba

Chanzo:ITV
 
Hawa si waliambiwa jogooo hapandi mtungi mpaka wanawake wao wakawa wana import toka Kenya, wametumia dawa gani?
 
Back
Top Bottom