Wanaume wa aina hii huchukiwa na wanawake

Wanaume wa aina hii huchukiwa na wanawake

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
++

Ni wanaume wasiotunza siri.

++
Pengine unaweza kushangaa sana.Kote duniani,mwanamke anajulikana kwa kutoficha siri.Hupenda kugawana siri za mahusiano ya wanaume wao mbele ya wenzao kama watu wanaokula sahani moja.Siri hizi hupeana saluni,vibarazani,ofisini na popote wakutanapo.LAKINI jambo hili likifanywa na wanaume,,wanawake huchukia sana.
++
Mwanasaikolojia Marabel Morgan anasema "....Wanaume wengi wasiofikiria wameharibu uhusiano mzuri na wake zao,kutokana na kuropoka siri za ndani za mke wake kwa rafiki zake.Kitu cha namna hiyo kinapomfikia mke wake,kitamfanya ajisikie kwamba amesalitiwa..."
++
Hivyo basi,wale wanaume wanaopenda kujigamba juu ya mapenzi,wafanye hivyo wakijua kuwa mwanamke ana uwezo mzuri wa kunusa habari,na hili akilijua uhusiano utaingia dosari.
++
Mambo madogo kama kuonyesha meseji zake,kuweka loudspeaker ili rafiki zako wasikie au mengineyo AKIJUA mwanamke au mchumba wako au mpenzi basi atakupunguzia alama fulani ktk kukuamini.
Kama yeye amesema basi ni yeye,,Mwache aseme kwani wao huishi kwa kutambiana juu ya jambo fulani kuhusu wenzi wao.Ukifanya hivyo mwanaume basi haufai.
Ni siri,,iweke hivyo
++
 
Ni ushamba/ujinga kumringishia mtu mambo ya ndoa yako ila ni busara kuomba ushauri pale unapokwama na kuona hauna njia nyngine yakufanya katika kulitatua jambo lililokusibu.
 
Back
Top Bottom