ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 664
Siku kadhaa zilizopita nilikuwa safarini Mbeya. Asubuhi wakati najiandaa kwenda kwenye michakato wale wadada wahudumu wakawa wanafua pale karibu na mlango wa chumba changu. wanaulizana wamehudumia mitaa mingapi usiku wa kuamkia siku hiyo. Wakimaanisha wameingia vyumba vingapi kutoa huduma ya ngono. Mmoja anasema yaani pale viungo vyote vinauma, amehudumia mitaa mitatu ila mtaa wa mwisho shughuli yake kidogo azimie kijamaa kilikuwa na ukame kweli. Mwingine anasema yeye ameenda mitaa miwili kwa nini ajitese wakati jana yake alipiga mitaa minne hivyo hela ya kula anayo. Sasa yule ambaye hata mimi nilikuwa nampigia hesabu akaniyeyusha (ilikuwa aje akanilinganisha kimavazi na wateja wa mitaa mingine akaona mi lazima naishi chini ya dola moja) akasema yeye amepiga mitaa sita hivo hajalala kabisa, lakini alihakikisha mitaa yote anatoa kimojakimoja tu. Akawasimulia alivonitosa wakacheeeeeka, nikafungua mlango nikatoka, kidogo azimie!!! Wakawa wadogooooo, mpaka nikafikiri sisimizi. Nikasepa zangu.