The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,155
Ndugu wanaume, fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya uzee wako. Sahau kuhusu watoto na mke wako! Kumbuka wewe peke yako ndiye mgeni (stranger) katika hiyo familia unayoiita yakwako. Kuna siku utabaini kuwa hiyo nyumba ni ya mke wako na watoto wako.
Mzee wa busara aliwahi kuniambia kuwa mwanaume ni sawa bulldozer au caterpillar linalotengeneza barabara nzuri za kuvutia. Lakini likishamakiza tu kutengeneza barabara haliruhusiwi kutembea tena juu ya barabara lililotengeneza lenyewe. Italetwa gari ya kubeba vitu vizito na kulibeba kisha kuliondoa kabisa barabarani kwa maelezo kuwa litaharibu barabara.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa wanaume wengi, unajinyima, unakopa, unavaa nguo kuukuu ili watoto wasome vizuri.
Lakini cha kusikitisha mtoto anapokuwa mtu mzima, Mama yao anaanza "kumlisha sumu" kuhusu wewe. Mke anaanza kuwalisha watoto sumu ya maneno ya uongo kuhusu baba yao. Abawapandikizia chuki ili waone wewe ulikuwa mtu mbaya na hukuwa msaada kwao. Utasikia akiwaambia watoto "kama sio Mimi kuhangaika ninyi msingesoma, baba yenu msimuone hivyo yeye hela yake ilikuwa ni kwa ajili ya wanawake na pombe." Hapo ujue greda linaanza kuondolewa kwenye barabara lililotengeneza lenyewe!
Watoto wanapoanza kujitegemea na kufanya kazi, huku baba yao akiwa ameshakuwa Mzee asiyeweza kufanya kazi ngumu na kama alikuwa ameajiriwa basi amestaafu.
Mtoto anapokuja kuwatembelea wazazi nyumbani, baba anapewa shilingi elfu 50 mbele ya Mama, wakati mama anamvutia mtoto wake jikoni na kumpa shilingi laki 1 ambayo baba hajui kama Mama amepewa.
Watoto wakishaondoka mke anamwambia mume akanunue sukari na mahitaji mengine. Huku mke akificha laki yake na kuitumia kwa mahitaji yake binafsi.
Hizi ni miongoni mwa sababu kwa nini wanaume wanakufa mapema kuliko wake zao.
Nimewaona wakina mama wakisafiri kwenda mjini na hata ng'ambo kuwatembelea watoto wao huku baba akiachwa nyumbani ahudumie kuku mbili na ng'ombe mbili, nikajiuliza kwa nini? Hatimaye nikapata kujua chanzo ni sumu kutoka kwa mke. Sumu ya kumchafua baba kwa watoto wake ni zaidi ya hukumu ya kifo!
Simama mwanaume, pambana kabla ya uzee haujakufika. Uzee ni baraka kama umejipanga mapema lakini uzee ni janga kama hukujiandaa kukabiliana na uzee! Mwenye sikio na asikie neno hili!