fantastic philip
Senior Member
- Oct 17, 2015
- 194
- 680
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa (R.E. 2019) kifungu cha 63, mume anatakiwa kumtunza mke wake kwa kuhakikisha anatafuta kipato na pia anamtunza vizuri nyumbani kwa kuhakikisha mke ameishi mahala pazuri na safi, kwakuhakikisha mke amepata chakula na sio vitu vya kupika, na pia kuhakikisha mke ana mavazi, yaani nguo zilizo tayari kuvaliwa.
Katika kuhakikisha hayo yanatimia, maana yake mume anatakiwa kuleta chakula kilichopikwa au kupika mwenyewe, mume anatakiwa kuhakikisha nyumba ni safi na inafaa kuishi, na pia mume anatakiwa kuhakikisha nguo za mke zimefuliwa. Sheria haijaeleza kwamba mke ana wajibu wa kupika, kusafisha nyumba, au kufua au kufanya kazi yoyote ya nyumbani.
Wajibu huo ni wa mwanaume, na kama mwanaume anaona amebanwa na majukumu basi anatakiwa kuajiri watu wa kufanya kazi hizo nyumbani kwaajili ya mke wake.
Hivyo basi dhana iliyozoeleka kwamba mwanamke ana wajibu wa kufanya kazi za nyumbani SIO KWELI kwa mujibu wa sheria.
Kutoka kwa @sheria.za.tanzania
Tuandikie maoni yako hapa