Wanaume tuwapende wanetu hasa wakike

cosa nostra

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,773
1,804
Hapa nchini kwetu katika familia nyingi suala la malezi mara nyingi huachiwa mama/mke na baba hujitoa kabisa katika suala hilo na kisingizia yuko busy kutafuta hela .

Ni kweli wanaume tumepewa jukumu la kutunza familia na Mungu lakini tunasahau kufuatilia maendelea ya watotot wetu ya kila siku hasa watoto wa kike wenye umri.

wanaume tumekua watu wakwanza kulaumu mke ikitokea mtoto anapata matatizo na kusahau kua sisi pia tuna jukumu la kua karibu na kujua maendeleo ya mtoto ya kila siku hata kama ni wakike,

Nawashauri wanaume wenzangu tukitoka kazini turudi kwanza nyumbani moja kujua kinachoendela nyumbani kabla watoto hawajalala ndio kama kwenda Bar au kupiga dili zingine za mtaani iwe baadae,

Wengi tunaogopa tukirudi nyumbani mke anakutia kitanzi na unakua huna sababu ya msingi ya kutoka jioni ndio maana wengi tunapitilizia bar na kwa michepuko na kurudi hoi,kitu ambacho mimi nakiona si vema kutoelewana na mkeo.

wanaume tukitoka asubuhi alfajiri nyumbani tunarudi usiku wa manane hivyo siku zote watoto. wanakua wanakusikia tu,kua baba amekuachia pesa ya viatu baba atakununulia hili na lile ila unasahau kua kulea mtoto si pesa na tumeshaona mifano mingi sana ya watoto walio haribika kimaadili kwa sababu ya pesa na kukosa malezi ya upande mmoja (baba)

[HASHTAG]#Tubadilike[/HASHTAG]

unnamed (27).jpg
 
Hilo la karudi nyumbani mapema ni gumu sana kwa hali ya maisha ya sasa inayokubidi kufanya kazi zaudi ya moja ili kuongeza kipato.Watoto walelewe tu mama yao mi ntakuwa napewa tu report na kuzipitia kama kuna kushauri ntafanya hivyo weekend ikibidi kutoa mkong'oto km kuna utovu wa nidhamu
 
Kuwa binadamu mwenye jinsia ya kiume hakukufanyi uwe na sifa ya kuwa baba.Jambo hili bahati mbaya sana ni wanawake wachache sana wanalijua na kulifuata......

Ukishaona mtu haoni umuhimu wa kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni na kujua wameshindaje na hata kusoma nini huyo ni binadamu tu mwenye jinsia ya kiume na hajui kabisa majukumu ya kuwa baba hivyo anakosa sifa ya kuwa baba.....

Kuwa na familia siyo fasheni bali ni kuongeza uwajibikaji....
 
ha ha ha
 
point
 
Back
Top Bottom