Sikuja duniani kuteseka mimi au kutesekea wengine.
Huu msemo wa wanaume tuliumbiwa mateso nilisha ukataa.
Watoto na mwanamke nitawajali kwa kiasi chao.
Lakini fungu kubwa, nguvu kubwa na jasho kubwa nimewekeza kwangu kwanza.
Kuwekeza nguvu kubwa kwa mke au watoto bila kujijaji wewe huo nao ni ujinga.
Watoto wakikua wataondoka kwangu nitabaki mwenyewe.
Sasa lazima ni enjoy jasho langu uzeeni kwa amani.
Watoto wataenda huko na wao watakuwa na maisha yao.