Wanaume tuna tatizo gani?

Omnilabeltech

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2026
Posts
394
Reaction score
573
Mfano mimi nikija hapa nikapost:

“Natafuta mwanamke wa kujenga naye maisha, mwenye malengo na anayejua anachotaka. Aliye serious ani-DM.”

Inawezekana kabisa DM yangu ikawa kavu kabisa .

Lakini mwanamke akipost kitu kama:

“Natafuta mwanaume wa kujenga naye maisha.”

Mara nyingi utaona comments na DM zikimiminika mpaka unajiuliza, hawa wanaume wote wametoka wapi?

Sasa swali langu ni:

Kwa nini mwanamke mmoja anaweza kupata approaches nyingi sana kutoka kwa wanaume, wakati mwanaume akijitangaza kutafuta mwanamke anaweza asipate response hata moja?

Je, ni kwamba wanaume ndio wengi wanaotafuta, au kuna sababu nyingine kama wanaume kutotambua thamani yao kwenye dating market?

Wanaume na wanawake, hebu tuambiane ukweli bila kuoneana aibu.
 
Uandishi wako tu hauwezi kuwavutia wanawake. Hawa warembo hawapendi wanaume waandike na vi imoj imoj vya kuchekacheka
 
Watu wanataka vipenyo tu mkuu hamna la zaidi
 
Umejuaje hilo? Umewahi kuja kwa ID ya kike na ya kiume kwa nyakati tofauti?
Anasema kuwa nyie mbona ni wabovu na mnajifanya kujiona wa thamani sana?

Ameongea kimafumbo tu huyu nadhani.

Anachozungumzia ni why mnaringa sana kukubali a watu wakati nyie ni wabovu kupindukia?
 
Lakini mwanamke akipost kitu kama:

“Natafuta mwanaume wa kujenga naye maisha.”

Mara nyingi utaona DM zikimiminika mpaka unajiuliza, hawa wanaume wote wametoka wapi?
Hili ulilijuaje?
 
Mwanamke akiku DM atakuombaje hela sasa?
Ebu fikiria wanawake 20 wakutake halafu wote wakuombe hela za gas, screen ya simu,, Kodi, Bibi mgonjwa NK wewe utafanyaje? Ndo maana hawaji wanataka wewe utongoze wakuombe hela.
 
Always, wanawake ni bidhaa adimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…