Wanaume tumekuwa dhaifu sana kwenye suala la Mapenzi

Wanaume/vijana wa kiume tumekuwa dhaifu sana kwenye suala la mapenzi.

Mwanaume unaenda kukutana na mwanamke kwa mara ya kwanza halafu wewe mwanaume ndo umejawa hofu na wasiwasi kuliko mwanamke mwenyewe!

Mwanaume unatongoza mwanamke kwa kulia lia na kujikombakomba kana kwamba anamuomba uhai!

Kuna wanaume wanarimotiwa na wake/wapenzi wao unaweza kusema wamerogwa kumbe ni wazima, hakuna cha limbwata ni ufala tu.

Wanawake kwasasa wanajiona matawi ya juu kwa sababu wanaabudiwa na baadhi ya wanaume!

Shida ni kutokujiamini/ kuendeshwa na hisia au ni nini?

Hivi ni kweli ujasiri wako, kujiamini kwako, akili zako zote na uanaume wako kwa ujumla, mbele ya Mwanamke ndo mwisho?

Shida kubwa ni hela mkuu ukiwa huna hela hata kutongoza ni changamoto.
 
Back
Top Bottom