Wanaume tuliooa Mungu atulinde

Wanaume tuliooa Mungu atulinde

Ndoa zina changamoto sana mazee. Hasahasa pale ambapo ulioa bila mkakati maalumu wa muda mrefu.
 
Habarini za jumapili wakuu..
Kwa sababu nimefika mwisho Naomba nilete hiki kisa hapa Leo. Kwa mwanaume kama mwanamke mzuri akikutaka ukachomoa asee wee Ni mwanaume haswaaa...

Iko hivi, mwaka juzi ilitokea nikachepuka nilileta kisa hapa na kuapa sitorudia ile kitu koz ilinitesa Sana. Mwaka huu nimejikuta katika mazingira magum Sana kuchomoka na hapa niseme waz kama nitavuka hapa nitashukuru Sana.

Kazin kwetu alikuja mfanyakazi mdada, kwa sura Ni mzuri kawaida... Sikua na mazoea naye, lkn siku moja ghafla aliniambia anajisikia vibaya anaomba msaada nimsogeze nyumbani, tulichukua pikipiki tulivofika sehem ambayo Haina watu alianza kulia Sana, Hali ile ilinilazimu kusimama kwa mda ili amalize kulia niendelee na safari.. alikua akisema anateseka Sana na ndoa yake na maisha yake, sikumuuliza kiundani Sana maana nilijua Ni changamoto za ndoa (coz na mm nimeoa), nikamfikisha karibu na kwake mie nikarudi zangu..

Kuanzia siku ile tulianza kuchati na kuwa marafiki wa kawaida. Nilijitaidi kumshaur na kumweka sawa ili aliendelee na familia yake maana alitaka kuvunja mji wake. Katika kushauri nilijikuta naingia katika uhusiano na yule Dada! So nikawa na mchepuko. Yule Dada alinipenda na nikajua ananipenda, mwanzon ilianza kama utani nikajikuta na mm nampenda tukaanza kuongea vizuri na kufanya mengi, japo ameolewa na mm nimeoa but tulijikuta tunapendana, nilianza kuona makosa mengi kwa wife maana niligundua kanizoe kiac kwamba ananichukulia for granted, japo hakua mzuri Sana lkn alionesha kuhitaji Sana mtu wa kumpa kampani na nilimpa that kampani. kweli alistahili kutreatiwa vile na mumewe maana Ni kiumbe complicated Sana kumhandle, panicking, matusi na lazy..

Kiukwelii moyoni nilikua naumia sana, Ila kutoka nashindwa, Nilikua Kila nikisali hili linakua ombi langu kwa Mungu anisaidie Sana niweze achana na hii kitu, alikula mda wangu na wakati mwingine mda wa wife.. but officially nimeamua kuvunja this relationship kwa msg Kali japo hata mm nasikia kummiss Mana Ni kama nimemzoea lkn sitaman kuendelea na hii kitu. Natamani niwe yule kwa mke wangu na familia yangu.

NB: Wanaume tuwe wema kwa wake zetu tunawaingiza matatizoni.
Wanawake wakti mwingine mwanaume anajikuta tu katika mazingira ya kuchepuka hata kama hajadhamiria, mtusamehe na kutuombea Sana.
Pole sana kwa mapito!

Mwenyezi Mungu asikie maombi yako na kukurudishia uanamume wako!
 
Ndoa ya kwanza ilikuwa ya Adam na Eva/Hawa...

Japo haikuwa na wifi, shemeji, mama mkwe, watoto wala wachepukaji ilivunjwa/iliingiliwa/ilivurugwa na nyoka (ibilisi).

Ukimjua adui wa jambo lako wanadamu hawakusumbui.
 
Msc. In Uchepukaji.... Hii shahada ni ngumu ...
 
Mna siku sita za kufanya kazi lakini si siku ya sabato.
 
Kwenye ndoa kuna changamoto zake, mitihani ya kuchepuka tunakutana nayo mingi mnoo ni vile tunakaza nafsi zetu.

Mtume(s.a.w)alituusia "mbora wenu ni mbora nyumbani mwake(mkewe/familia)
Uchawi mkubwa kabisa ndani ya ndoa ni mazoea, huwa tunajisahau(ke kwa me) mkianza kuchukuliana poa poa, basi hapo ndio tabu inaanzia, kila kitu poa poa, kuanzia kulala, tendo, matukio muhimu(kukoga, kula etc) hapo ndio ndoa inaanza kulega sasa ukikutana na mchepuko, kawaida ya mapenzi mwanzoni yananoga lazima uzamie kwenye kibanda hasara.

Kikubwa ni kutuliza nafsi zetu, tutizame tunachokifanya nini faida yake na madhara yake.
 
Mungu awabariki wanaume wenye kuheshimu ndoa zao.
Sorry wote ndio tuko hivi
IMG_20210924_074847.jpg
 
Hata ukienda kununua parachichi sokoni lazima ubonyeze bonyeze kadhaa.
Hongera mkuu, lakini inaonekana kidonda bado kibichi. Sitashangaa kama ukifuata cha mwagano.
 
Na ubaya ni kwamba ukishaoa ndio unaona KILA kona ukipita unakutana na wadada wazur tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kemea toka pepo shenzi kabisa
 
Back
Top Bottom