Ni kitu kizuri sanaMimi huwa napenda kumsindikiza mke wangu clinic ya ujauzito hadi clinic ya mtoto
vya bure ghali mzee.....Natumai mko vema ndugu.
Kama mada inavyojieleza hapo juu, ni rai yangu kwetu akina baba na baba watarajiwa kuambatana na wake zetu waendapo kliniki za ujauzito hasa kwenye hospitali au vituo vya afya vya serikali manake bila hivyo wake zetu wanapata shida na kutia huruma sana.
Jana nilimpeleka wife kliniki ktk kituo kimoja cha afya cha serikali,nilipofika pale nilikuta akina mama tu wamechoka kishenzi kutokana na matumbo yao. Tulichelewa kufika pale ila wale tuliowakuta walionekana walifika toka asubuhi mana walikuwa wanalalamika sana.
Basi tulipofika Mimi na wife Nesi akatuuliza "ninyi ni baba na mama"? niliposema ndio, pamoja na kwamba tulichelewa kufika pale na tuliwakuta akina Dada/mama wengi tukaambiwa tupite moja kwa moja kupatiwa huduma. Jinsi walivyolalamika wale watu niliumia sana.
Nilipoingia kule ndani nikamuuliza Nesi kwa nini ametutaka tuingie moja kwa moja bila kufata foleni? Akanijibu kwamba utaratibu Wa kwenda kliniki ni baba na mama waambatane,na kama baba amesafiri,hayupo au anaumwa basi mama aambatane na barua toka kwa Mwenyekiti Wa serikali ya mtaa.
Akamalizia kwa kusema asiyetaka masharti ya serikali aende hospitali binafsi, haiwezekani kila siku akina baba wawaache wake zao peke yao wakati suala la ulezi Wa ujauzito na kufuatilia afya ya kiumbe cha tumboni na mama ni jukumu la wote, na kila siku tunawaambia!
Yaweza kuwa si vituo vyote vya afya vya serikali wanafanya hivyo ila ni vema pale inapobidi tusaidiane na wake zetu,wanateseka jamani hasa zinapotokea adha kama hizo.
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]Dah....unamsindikiza halafu mwenye zigo lake anakuangalia kwa dirishani....anacheeeka...ni wazo tu... tofauti....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umewaza kama mimi mkuuDah....unamsindikiza halafu mwenye zigo lake anakuangalia kwa dirishani....anacheeeka...ni wazo tu... tofauti....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Umewaza kama mimi mkuu
Twende mbele turudi nyuma, kikwazo kikubwa cha wanaume kutowasindikiza wake zao Clinic pindi wawapo wajawazito ni suala la upimaji wa Virusi vya Ukimwi. Only that!!
Ha ha ha nyie watu nyieDah....unamsindikiza halafu mwenye zigo lake anakuangalia kwa dirishani....anacheeeka...ni wazo tu... tofauti....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sawavya bure ghali mzee.....
Na nasikia ukiongozana naye, unapewa kipaumbele......wish nikifika hatua hiyo nitambebea mkoba twende pamojaNatumai mko vema ndugu.
Kama mada inavyojieleza hapo juu, ni rai yangu kwetu akina baba na baba watarajiwa kuambatana na wake zetu waendapo kliniki za ujauzito hasa kwenye hospitali au vituo vya afya vya serikali manake bila hivyo wake zetu wanapata shida na kutia huruma sana.
Jana nilimpeleka wife kliniki ktk kituo kimoja cha afya cha serikali,nilipofika pale nilikuta akina mama tu wamechoka kishenzi kutokana na matumbo yao. Tulichelewa kufika pale ila wale tuliowakuta walionekana walifika toka asubuhi mana walikuwa wanalalamika sana.
Basi tulipofika Mimi na wife Nesi akatuuliza "ninyi ni baba na mama"? niliposema ndio, pamoja na kwamba tulichelewa kufika pale na tuliwakuta akina Dada/mama wengi tukaambiwa tupite moja kwa moja kupatiwa huduma. Jinsi walivyolalamika wale watu niliumia sana.
Nilipoingia kule ndani nikamuuliza Nesi kwa nini ametutaka tuingie moja kwa moja bila kufata foleni? Akanijibu kwamba utaratibu Wa kwenda kliniki ni baba na mama waambatane,na kama baba amesafiri,hayupo au anaumwa basi mama aambatane na barua toka kwa Mwenyekiti Wa serikali ya mtaa.
Akamalizia kwa kusema asiyetaka masharti ya serikali aende hospitali binafsi, haiwezekani kila siku akina baba wawaache wake zao peke yao wakati suala la ulezi Wa ujauzito na kufuatilia afya ya kiumbe cha tumboni na mama ni jukumu la wote, na kila siku tunawaambia!
Yaweza kuwa si vituo vyote vya afya vya serikali wanafanya hivyo ila ni vema pale inapobidi tusaidiane na wake zetu,wanateseka jamani hasa zinapotokea adha kama hizo.
Ndio iko hivyo ndio maana hata Mimi nilichelewa kufika pale lakini nilipofika tu Nesi akasema we mama uliyekuja na baba njooni mpewe huduma muendelee na shughuli zenu.Na nasikia ukiongozana naye, unapewa kipaumbele......wish nikifika hatua hiyo nitambebea mkoba twende pamoja