Wanaume tuambatane na wake zetu kliniki

Wanaume tuambatane na wake zetu kliniki

severinembena

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Posts
2,435
Reaction score
2,404
Natumai mko vema ndugu.

Kama mada inavyojieleza hapo juu, ni rai yangu kwetu akina baba na baba watarajiwa kuambatana na wake zetu waendapo kliniki za ujauzito hasa kwenye hospitali au vituo vya afya vya serikali manake bila hivyo wake zetu wanapata shida na kutia huruma sana.

Jana nilimpeleka wife kliniki ktk kituo kimoja cha afya cha serikali,nilipofika pale nilikuta akina mama tu wamechoka kishenzi kutokana na matumbo yao. Tulichelewa kufika pale ila wale tuliowakuta walionekana walifika toka asubuhi mana walikuwa wanalalamika sana.

Basi tulipofika Mimi na wife Nesi akatuuliza "ninyi ni baba na mama"? niliposema ndio, pamoja na kwamba tulichelewa kufika pale na tuliwakuta akina Dada/mama wengi tukaambiwa tupite moja kwa moja kupatiwa huduma. Jinsi walivyolalamika wale watu niliumia sana.

Nilipoingia kule ndani nikamuuliza Nesi kwa nini ametutaka tuingie moja kwa moja bila kufata foleni? Akanijibu kwamba utaratibu Wa kwenda kliniki ni baba na mama waambatane,na kama baba amesafiri,hayupo au anaumwa basi mama aambatane na barua toka kwa Mwenyekiti Wa serikali ya mtaa.

Akamalizia kwa kusema asiyetaka masharti ya serikali aende hospitali binafsi, haiwezekani kila siku akina baba wawaache wake zao peke yao wakati suala la ulezi Wa ujauzito na kufuatilia afya ya kiumbe cha tumboni na mama ni jukumu la wote, na kila siku tunawaambia!

Yaweza kuwa si vituo vyote vya afya vya serikali wanafanya hivyo ila ni vema pale inapobidi tusaidiane na wake zetu,wanateseka jamani hasa zinapotokea adha kama hizo.
 
Wanaume wengi wanaogopa kwenda Clinic na wake zao wakidhani watapimwa Naniliu,wasindikizeni wake zenu jamani,kupima ni hiari ya mtu.
 
Vizuri kwa kuwajuza manjuka wenzio huko sisi ni zilipendwa mtoto wa mwisho yupo form two.
 
Wanaume wengi wanaogopa kwenda Clinic na wake zao wakidhani watapimwa Naniliu,wasindikizeni wake zenu jamani,kupima ni hiari ya mtu.
Daa ila kuna kamtihani asee sasa hivi sehemu nyingi mama anapoanza clinic ni lazima yeye na baba wapimwe naniliu
 
Ni vema,endelea tu bro ni heri sana
Ni kitu kizuri kwanza wanajisikia kuthaminiwa, kuwa katika ulinzi na pia wanakuwa na furaha. Tuungane nao katika hayo machungu ya kulea mimba, maana wengine wakiwa na mimba wanatia huruma, wanogopa, safari ya miezi tisa sio mchezo.
 
Back
Top Bottom