Wanaume tuache Ubinafsi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
WANAUME TUACHE UBINAFSI!

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

Nilikuwa natoka Mashariki kuelekea Magharibi, sasa nitatokea Magharibi kurudi Mashariki. Kaskazini kwenda kusini kisha , kusini kurejea Kaskazini kama pepo za Kusi. Hivyo ndivyo safari yangu ilivyo.

Niite Taikon wa Fasihi, Kutoka Nyota ya Tibeli

Tabia ya ubinafsi imezidi kushamiri Sana kadiri siku zinavyosonga. Hii ni kusema kuwa Upendo siku hizi unayoyoma. Kwa maana kwenye upendo hakuna msamiati Ubinafsi.

Ubinafsi ni kitendo au hali au tabia ya kujipendelea kuliko pitiliza bila kujali Watu wengine.
Mtu yeyote anayejipenda kuliko pitiliza kamwe hawezi kukupenda, Kwa sababu MTU huyo ni mbinafsi.
Mtu mbinafsi hawezi kukupenda ingawaje atakuwa anakudanganya anakupenda.

Mtu mbinafsi hujiangalie yeye tuu bila kuangalia shida za Watu wengine,

Kwa mfano, mtu anaweza kuvuta sigara ndani ya Daladala, haoni kuwa Kwa wenzake ni kero, yeye anajijali mwenyewe MTU huyo ni mbinafsi, Hana upendo Kwa wengine Ila anajipendelea mwenyewe tuu.

Au mtu yupo nyumbani hasa nyumba ya Kupanga, anawasha muziki Kwa Sauti ya juu bila kujali kuwa anawakera Watu wengine mtu hiyo yupo kundi la Watu wabinafsi.
Hii itaenda sambamba na makanisa ya kilokole yanayopiga Makelele kucha kutwa huku yakizua usumbufu na uchafuzi wa mazingira, Sisi tutasema Makanisa hayo yanaubinafsi, yanajijali yenyewe bila kuangalia Watu wengine.

Ubinafsi ni kosa katika sheria za dini Kwa sababu huwezi kuwa mbinafsi alafu ukawa na upendo.
Ubinafsi pia ni kosa katika Asili(nature) Kwa sababu utazua matatizo ya kimahusiano baina ya mtu na mtu, au MTU na mazingira.

Tukirudi kwenye mada yetu ambayo itahusu ubinafsi wa Sisi wanaume ambao kimsingi tunatakiwa kuuacha mara Moja.

I) Ubinafsi wa Chakula.
Sijajua kama ni umaskini au ni kitu gani katika Aina Hii ya ubinafsi.
Baadhi ya wanaume tunapenda kuwekewa vile vyakula vizuri zuri na minofu mikubwa ya nyama mathalani Mapaja, kidari n.k. Huku tukiwaachia Wanawake na watoto wale vipapatio na vile finyango vidogo vidogo. Ukifuatilia sababu za hayo kufanyika haina hata mantiki.

Baba mwenye upendo anajua kabisa ndani ya familia kila mmoja anayohaki ya Kula chakula kizuri, kuanzia mke mpaka Watoto. Hivyo ni jukumu la Baba kufanya kazi Kwa bidii kuhakikisha anapata chakula cha kutosha ili kila mwanafamilia apate kitu Kizuri, wote wale mapaja.

Ikiwa uwezo utakuwa mdogo kulingana na majaliwa basi itabidi uundwe utaratibu wa kuwekeana zamu, leo Fulani na Fulani mtakula Paja, Wakati mwingine itakuwa Fulani na Fulani, hivyohivyo mpaka wote muishe.
Hivyo ndivyo familia inavyojengwa Kwa Upendo.

Vinginevyo MKE yeye mwenyewe Kwa vile ndiye incharge wa mambo ya mapishi na shughuli zingine za nyumbani, yeye ndio aseme Kwa mapenzi yake, akiwaambia Watoto Jamani Hiki ni chakula cha Baba yenu,
Alafu Baba ukija Kutoka mizunguko yako, lazima uwe Gentleman, unaweza kusema; ooh! Chakula cha leo kinaharufu nzuri, embu!(unaonja) oooh! Nikitamu pia, unamtazamo Mkeo unamwambia wewe ni fundi, unajua mpaka unajua tena. Unamkonyeza kichokozi kisha unambusu Kwa mbali,

Unachukua mnofu mmoja unampa mtoto, mtoto anapokea, Mkeo anamkanya mtoto, unasisitiza Acha mtoto ale, Mkeo anakaza, unamkatia kipande kidogo mtoto ale.
Au kama ni wale wa Kula Kwa pamoja, Mkeo kakuwekea minofu mikubwa, basi wewe unampunguzia sehemu ya Ile minofu.

Halikadhalika Mwanamke akiwa na minofu atampunguzia mumewe. Hiyo tunaita Love.

ii) Ubinafsi wa Kihisia.
Hii ndio Ipo Sana.
Wanaume lazima tuelewe, vile tunavyoumia Wakati Wake zetu wanatongozwa au kuchapwa na kubenjuliwa na wahuni ndivyo Wanawake wanavyoumia tukiwa-cheat.
Ipo kasumba na dhana potofu kuwa Sisi wanaume tunatamaa ni kweli tunatamaa ndio maana tukaambiwa tuoe Mwanamke mzuri kadiri ya vigezo vyetu ili hizo tamaa za mwili huyo Mwanamke azikomeshe.
(Sisemi hapa kama MTU Mwema) nazungumzia ubinafsi wetu kama wanaume.

Ni ubinafsi wa Hali ya juu kutokuthamini hisia za wengine hasa Mkeo na watoto.
Unajali hisia zako pekee, vile zitakavyokutuma unazifuata.
Alafu muda huohuo unaumia Mkeo akitoka nje. Huo ni upunguani.

Au unakuta kijana anampotezea muda Binti WA watu huku akijua kabisa hatamuoa, huo ni ubinafsi wa Hali ya juu.
Mtu kama hutomuoa mwambie Mimi sitakuoa, mtongoze demu mwambie ukweli wote, mwambie umemtamani, yeye ni mzuri, na unataka mapenzi yake. Ila hauna Mpango WA kumuoa.
Kama yupo interested na mahusiano ya namna hiyo atakukubalia, au atakataa kama hayupo tayari kuingia kwenye relationship ya hivyo.

Mbona Sisi wengine tupo wazi na tunapewa tuu bila hiyana,,, Kuliko umdhulumu MTU ni Bora umwambie ukweli, uamuzi ubakie kwake.

iii) Ubinafsi wa kusosholaizi
Wewe ndiye unataka utumie mitandao pekeako, wewe ndio unataka ukiwa nyumbani chaneli uipendayo uonyeshwe, wewe ndiye unajitoa out pekeako mara Bar Hii mara Ile, wewe pekeako ndio unandugu na marafiki. Come on!
Kisingizio chako ni oooh! nikimpa Uhuru MKE wangu nitachapiwa😂😂😂
Hizo ni Akili au Matope.
Kuchapiwa kunategemea na Akili na tabia ya Mwanamke.
Hata akiwa nyumbani au umfunge jela awe pekeake akiamua kuchapwa atachapwa tuu.

Ubinafsi ni pamoja kutaka kummiliki. Mwenzako kama Kandambili zako, yaani kama Mfugo wako.

Wekeni sheria, Kanuni na Standards za familia yenu. Kisha kila MTU awe huru kuishi Maisha yake Kwa furaha ndani ya Ndoa yenu.
Kama zitavunjwa hizo Kanuni hasa zile sheria kubwakubwa basi itamkwe kabisa kuwa Ndoa itavunjwa.
Rahisi Sana.
Kuliko umnyime mwenzako Uhuru Kwa kumbana kisa ubinafsi wako.
Huko ni kutokujiamini

Ubinafsi ni pamoja na kutaka kuidhibiti Free Will ya MTU mwingine.

Familia nyingi na ndoa nyingi zinaanguka Kwa sababu ya ubinafsi uliopitiliza ya wenza ndani ya Ndoa.

Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Robert, unaweza kueleza ni kwanini uzi wako una comments 4 hadi sasa toka muda ulioanzishwa? Hii ni tofauti kabisa na nyuzi za kuwarekebisha/kosoa wanawake.

This says alot juu ya mwanaume wa wakati huu.
 
🤣🤣🤣🤣

Inaweza toa tafsiri kuwa, Wanawake sio wepesi wa kushambulia wanaume mitandaoni.
Pia inaonyesha Wanawake sio wepesi kujitetea na kupinga Tabia Mbaya za Wanaume.
 
Hivi inakuwaje mwanaume mwenye familia unajipigilia misosi mikali huko kwenye mihangaiko yako,halafu hata siku moja moja hufungashi mapocho pocho uende nayo nyumbani nao wakafaidi, Sawa mke unaweza mchukulia poa lkn vipi kuhusu wanao WA damu?

Seriously kabisa unainjoy wakati wanao unajua kabisa hawapati hayo mambo matamu, hapana wazee tunafeli Sana ebu tubadilike na kujali familia zetu pia, wakati mwingine hatupati mambo matamu toka Kwa vipenzi vyetu kwasababu ya ubinafsi.
 
Pengine ni kweli, kuna kaka alinijibu humu kuwa si huwa mnatusema sana mnapokuwa saluni na kwenye vicoba?

Kweli kabisa saluni na vicobani tunakuwaga na majambo yetu.
 
Robert, unaweza kueleza ni kwanini uzi wako una comments 4 hadi sasa toka muda ulioanzishwa? Hii ni tofauti kabisa na nyuzi za kuwarekebisha/kosoa wanawake.

This says alot juu ya mwanaume wa wakati huu.
Hakika.
Wangekuwa washatokwa povu sio la nchi hii, na uzi ungekuwa page ya 500.
 
Hivi inakuwaje mwanaume mwenye familia unajipigilia misosi mikali huko kwenye mihangaiko yako,halafu hata siku moja moja hufungashi mapocho pocho uende nayo nyumbani nao wakafaidi, Sawa mke unaweza mchukulia poa lkn vipi kuhusu wanao WA damu?

Seriously kabisa unainjoy wakati wanao unajua kabisa hawapati hayo mambo matamu, hapana wazee tunafeli Sana ebu tubadilike na kujali familia zetu pia, wakati mwingine hatupati mambo matamu toka Kwa vipenzi vyetu kwasababu ya ubinafsi.

Mbona hiyo ipo Sana.
Sema Vijana WA siku hizi wanajitahidi kujali
 
Robert, unaweza kueleza ni kwanini uzi wako una comments 4 hadi sasa toka muda ulioanzishwa? Hii ni tofauti kabisa na nyuzi za kuwarekebisha/kosoa wanawake.

This says alot juu ya mwanaume wa wakati huu.
Sasa wewe umekuja kusoma ujumbe na kutoa maoni yako au umekuja kulaumu mleta mada kwann uzi wake una comment chache kutoka kwa wanaume?

Sasa kimsingi ukiona kimya jua ujumbe umefika na umewaingia walengwa na ndio wanautafakari kwa maana wanachakata maneno yaliyopo ndani ya huo uzi.

Sasa ulitaka waongee nini na wanasikiliza na kudigest walichoambiwa.
 
Sasa, Sasa, Sasa... Usijali Robert mwenyewe amenielewa nilichouliza. Ilikuwa ni observation yangu tu...
 
Hivi inakuwaje mwanaume mwenye familia unajipigilia misosi mikali huko kwenye mihangaiko yako,halafu hata siku moja moja hufungashi mapocho pocho uende nayo nyumbani nao wakafaidi, Sawa mke unaweza mchukulia poa lkn vipi kuhusu wanao WA damu?

Seriously kabisa unainjoy wakati wanao unajua kabisa hawapati hayo mambo matamu, hapana wazee tunafeli Sana ebu tubadilike na kujali familia zetu pia, wakati mwingine hatupati mambo matamu toka Kwa vipenzi vyetu kwasababu ya ubinafsi.
Kwa uchunguzi wangu nimegundua wanaume huwa hawapati muda wa kuenjoy uhuru bila majukumu na kuweza kufurahia vipato vyao ikiwamo kula vema.

Unakuta kijana anaishi kwao kwa kubanwa banwa, msosi wa kengele, na bado akila hafurahii maana ni kila siku bamia, dagaa chukuchuku, mara matembele hafurahii msosi anaokula.

Na bado akianikiwa kupata kazi ghafla bin voop mwanamke huyu ameshakuja ameshamtegea ujauzito ndani ya miezi miwili tu ya kuishi pamoja kisha hapo hapo atataka ndoa ya haraka kisha story inayofuata ni majukumu mapya ambapo pesa itaishia kwenye majukumu ya lea familia yake ya mke na watoto, bado wazazi wake na ndugu hawajaja kuomba misaada na upande wa mke wake napo wanamjia juu kuomba sapoti.

So anajikuta yupo katikati hana direction wala uwezo wa kuenjoy life ndio maana wanaamua kuwa selfish aidha atafute nyumba ndogo pembeni awe anaenda kupikiwa vizuri huko na kula vizuri ili at least afurahie maisha au atakuwa ni mtu wa kwenda pubs na kula vema maana kama mkewe asipomuandalia vizuri basi inakuwa mtihani yeye kula nyumbani.

Me nashauri kwa mtoto wa kiume ukiona umefanikiwa kupata Kazi ya kukupa kipato kwa maana ya Ajira au kupata biashara nzuri then nakushauri tenga at least miaka yako mitatu ambayo utaishi wewe kama wewe pekee yako huku ukiwa makini sana na matumizi ya pesa zako maana upo pekee yako so ni ngumu sana kuziharibu.

Nunua assets zako za ndani ambazo utahitaji kujipa furaha mfano entertainment gears kama TV ya kisasa, home theater, friji ya kuweka vinywaji na vyakula, sofa nzuri, picha nzuri za ukutani etc. Hii itakufanya kuwa na sehemu ya kufurahia (a home ) na kupata utulivu wako. Then kuwa focused kwenye kutunza pesa zako na kuwekeza pahala salama zisipotee.

Hakikisha unakula vizuri na kujaribu kila chakula ambacho ungetamani kukila hapa duniani. Kula ni ibada especially kwetu sisi wanaume. Chakula ni kitu ambacho kimeshikamana na roho zetu. So nenda supermarket kanunue vyakula unapenda mfano ice cream, nyama, cereals, soda, juice, sausages, nyama ya kusaga, nenda kwenye cafeteria nunua hot chocolate, cappuccino, latte, mochaccino, milkshakes, yaani wewe hakikisha unaenjoy kutafuna na kunywa vyakula vipya na kuvifurahia kwa uhuru. Nunua nyama mbali mbali mfano, kuku, samaki wa aina mbali mbali, uwe nao ndani na kuwapika kila unapopata hamu.

Jaza friji na vyakula na vinywaji vizuri kisha uvitumie kwa kuvifurahia. Hii itakusaidia kufurahia uhuru wa chakula na kuvizoea na kuveenjoy. Hii itakusaidia hata muda utakaposema sasa nataka nioe nianzishe familia nafsi inakuwa tayari imezoea hivi vitu na utapenda kumletea mkeo na watoto pia wavifurahie.

Hii formula inafanya kazi katika misingi ya exposure. Wanasema jambo ambalo wewe umeshawahi lipitia aidha la kufurahisha au la kuumiza basi automatically na subconsciously bila kujijua utataka na watoto au mkeo apitie.
Umeshakutana na wale wazee wanapesa ila nyumbani kwake mke na watoto wanakula kande tena zile chukuchuku hazina hata nazi.
Ukidadisi kwann anakwambia anawafundisha maisha sababu yeye mwenyewe aliishi hivyo utotoni so anakuwa kama anaona kuwapa watoto wake maisha ya furaha na kupata vitu ambavyo yeye hakupata utotoni basi ni kujidhurumu nafsi na kuwaendekeza watoto kwa kuwapa vitu ambavyo si vya lazima.

So ukiwa na exposure ni ngumu sana kuwanyima watoto vitu vidogo kama chakula kizuri. Ndio maana nasema kama ulikosa maisha ya kula kuku wiki nzima, kunywa chai ya maziwa, mkate wa siagi na mayai na sausage, kubadili mboga saba kila siku then tenga muda wa kujipa hii exposure pekee yako ili ufurahie na kuzoea. Ukija kuwa na familia utaona namna itakavyokuwa ni kazi rahisi kila siku kurejea na kifurushi cha hivi vitu na mkeo na watoto kufurahia maisha.

Unarudi home pitia Azam pale nunua lile limkebe la lita tano la Ice cream, pitia kule sokoni kachukue kuku wa kutosha kila mtu hapo nyumbani kupata nusu kuku. Pitia feri nunua samaki kwa bei ya jumla vipande vya kutosha kila mtu kula akatosheka.

Nunua soda crate mbili at least kila baada ya wiki mbili (weka tahadhali hapa watoto wanywe kwa utaratibu sio kunywa soda kama maji ya kunywa si nzuri kiafya),agiza wale watengeneza keki wakutengenezee keki nzuri na tamu kwaajiri ya dinner hapo nyumbani keki nzuri unapata hata kwa bajeti kati ya 15,000 hadi 50,000 ni wewe tu uwezo wako.

Hivi vitu ukivifanya kwa familia yako utaona namna watoto watakavyokuwa na furaha na mama yao lakini pia utawapa exposure ya chakula ambayo itawafanya wajifunze ulaji bila mipaka. Sio unakuwa na familia wakiona kuku wanahisi ni chakula cha sikukuu, chipsi ni anasa, soda ni anasa, keki ni hadi birthday au harusi, Ice cream ni hadi ukitoka out, haya mambo si ya kuwajenga nayo watoto.
 
Chief

Kwanza aanza na hizo 🍿🍿🍿 hlf kuhusu kinywaji mangi atahusika

Umeongea mambo makubwa Sana ambayo yanajenga na kubadilisha Maisha yetu.

Uishi maisha marefu chief

🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom