Wanaume tuache kulalamika ovyo

IKARAHANSI

JF-Expert Member
Jul 30, 2019
398
479
Habari waheshimiwa!!

Nimekuwa nikisikia na kusoma mara kwa mara wanaume wakilalamikiwa na wanawake kuwa hawawaridhishi katika mambo mbalimbali. baada ya kufanya uchunguzi binafsi niligundua yafuatayo:-

Mosi: Kuna usemi unasema kuwa wanawake ni viumbe dhaifu hivyo tuishi navyo kwa akili, hii naithibitisha kila siku kwa kuwaona wanawake ambao wao waliumbwa toleo la pili baada ya wanaume(waliumbwa vizuri kuliko sisi wanaume) lakini cha ajabu eti wanataka usawa (kuwa sawa na sisi). Kinachonikera zaidi eti kuna baadhi ya wanaume nao wanataka kwenda sambamba na wanawake hawa.

Pili: Ukizaliwa Mwanaume basi unatakiwa kujua kuwa wewe ni kiongozi, yaani ukishindwa kuongoza taasisi, nchi au shirika basi utaongoza familia (labda usioe au uwe hanithi). Kazi ya kiongozi mahali popote duniani inafahamika kuwa ni kuhakikisha jamii anayoiongoza inapata mahitaji muhimu kwa kadri atakavyojaliwa kiuwezo na kuwa na upendo kwa watu wake, lakini baadhi ya wanaume wamekuwa wakilalama tu bila kufanya kazi matokeo yake kusababisha kudharaulika kwa wake zao na ndugu zao.

Tatu: Napenda kuwaasa wanaume wenzangu kuwa sisi tumezaliwa kupambana na ndiyo maana hata maisha yetu ni mafupi kuliko wao (Wanawake) pia hata viungo vyetu vya uzazi vimeumbwa kutoa zaidi kuliko kupokea na vile vya kike vimeumbwa kupokea zaidi na kutoa mara chache. Sasa basi yatupasa kufanya kazi zaidi ili kustawisha uchumi wa familia. MALALAMIKO yakizidi huleta dharau hasa kama unapenda kulalamika mbele ya wanawake.

Haya mambo ya kuitwa eti una kibamia, mara humridhishi huletwa na hali mbaya ya uchumi (ukosefu wa fedha) ukiwa na fedha ya kukidhi mahitaji yako na yake ni aghalabu kusikia kauli kama hizo (hata kama utakuwa na kibamia) atakuvumilia tu. WANAUME TUCHAPE KAZI MALALAMIKO YAKIZIDI HUPOTEZA MUDA.
 
Back
Top Bottom