Wanaume na kupunguzwa macho

Vaislay

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
4,532
1,819
Natumai wote tu wazima kwa uwezo wa mola.....:wave:
Kuna jambo huwa nikikumbuka linanifurahisha sana japo siku ya kwanza nilipata mshituko kidogo.
Home kulikuwa na housegirl aliezaliwa 1994,katika stori akawa ananiambia.

"Dada mimi nikimpata mwanaume kama anamacho matatu nampunguza moja, kama ana manne nampunguza yote abaki na jicho moja alilozaliwa nalo toka kwa mama yake",...Nilijikuta nacheka, nae akakazia "unadhani nakutania yani sitaki masihara kabisa".

ikabidi nimuulize kwani we sahizi hakuna anaekubandua?akajibu aah hawa watoto hawa bado hawana mawazo mi naitaka ile mijitu yenye mawazo yao, NILICHOKA.

nikajiuliza huyu mtoto mambo ya kupunguza wanaume macho kayapatia wapi,na hapo ndo kwanza ana kumi na...je akiwa na 20 na...si balaa hili.Kwa stail hii wanaume mtapona kweli si mtageuzwa mazezeta mpaka mkome, Nawaonea huruma sana kaka zangu mana inaonekana mmepaniwa, hasa wale wenye wenye macho matatu au manne......Bora muanze kujipunguza macho wenyewe kuliko kusubiri kupunguzwa.:yield:
 
Aje anipunguze mie aone kama hatojipunguza yeye. Mambo hayo yashapitwa na wakati, upendo wa kweli 2 ndo unapunguza macho.
 
Huyo anaonekana utoto unaendana nae na machepele mengi.
Akikua na akijapata mkuno mujarabb , kwa maana ya kukunwa chepele lote titamuondoka na pyerepyere zitamuisha kinywani.
 
Wameshindwa mashangingi walokubuhu ununda ataweza yeye? hao viumbe wala sio wakuwakamia chamsingi amuombe mungu ampe mwenye kheir na yeye...
 
aisee mpaka sasa sijaambulia kitu hapa...kupunguzwa macho ndo nini..ah na mi nilidhani najua kiswahili fika
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom