Wanaume mnashangaza sana

Asante umeamua kutufichia siri ,lakini ukweli ni kwamba
wanaowananga single mums wapo humu humu.
natamani kabla ya mtu kulaumu ni vyema
wakatafuta sababu ya ni kwa nini mtu ana hali hiyo
aliyonayo.
 
Sio single mothers wote wamezalishwa na waume za watu
Jaribuni kuwaheshimu hawa watu jamani afterall wana maumivu makali ya kuachiwa mzigo na wenzi wao.
Alafu kabla hujatoa uchafu wowote kupitia kinywa chako kumbuka kuna karma
 
Ndo napowashangaaga yaani mtu mwanamke hana bikira kwake safi ila aliyezaa hapana sasa tofauti ipo wapi kati ya aliyezaa na aliyekwisha fanya uzinzi, ndipo naposemaga hutaki singo mother basi kataa na aliyekwisha fanya uzinzi ila hakubatika kupata mtoto vinginevyo anayekataa single mother nakukubali asiye na bikiri sina budi kumuita kichaa, afu kuna bikira feki pia siku hizi
 
Nafikiri umenisaidia kufikisha ujumbe kwa lugha nyepesi mana uandishi na uongeaji ni taaluma u ger ma point thankiu kunywa soda hapo kw mangi
 
Point
 
Afadhali mnatokea mara moja moja kuwapa somo wadogo zenu.
 
Mleta mada naomba utambue kwamba, akuna mwanaume mwenye akili zake timamu, atakayeweza kumnyanyapaa mwanamke eti kisa ni "single mother".... Kwa sababu katika jamii nyingi tunazoishi, ni wazi kwamba katika familia 10 za mtaa mmoja, kuna uwezekana mkubwa wa kukuta familia 4-7 zinaendeshwa na single mothers hao hao tunawazungumzia hapa. Hivyo basi kila mwanaume anayemuona, ni wazi anao uhusiano kwa namna moja ama nyingine na hao single mother(s). inawezekana akawa ni mama yake, dada, shangazi n.k. Hivyo sio rahisi kuwadharau kwa namna yoyote ile....

Ukweli uliopo ni kwamba, asilimia 85 ya single mothers wa kileo, ni wale waliozalishwa na kutelekezwa na wanaume zao....na ukichunguza kwa umakini, utagundua chanzo, ni hii tabia walionayo wanawake wengi wa kileo ya "vuta nikuvute".... yaani tabia ya kushindwa kuishi katika misingi ya kiuwanamke wa kiafrika(wapo wanaoielewa), na hatimahe kuwa ni watu wa kutwa, wao kugombana na waume zao tu. Sasa kwa kawaida sisi wanaume sio rahisi kukaa na mwanamke wa aina hiyo, na hatimahe mwanamke huyo ujikuta akikikimbiwa.....mwisho anaishia kuishi maisha ya upweke, kuchukia wanaume, majuto, na wengine kuishi katika mazingira magumu mno(kiumaskini).

Sasa tatizo linakuja pale, huyo single mother (s) anakutana na mwanaume, kisha anaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na huyo mwanaume..... Usually kuna asilimia 30 tu, za kusema hao watu wataweza kuishi kwa amani. Lakini asilimia zote 70 zilizobakia hapo, kuna uwezekana mkubwa wa kushindwa kwa hao watu kuishi kwa amani. Maana huyo mwanamke anakuwa ameathirika kisaikolojia, hivyo sio rahisi kuwa sawa 100%, na ukikuta huyo mwanamke ni wa type za "vuta nikute" usually huyo mwanaume lazima pia ashindwe kukaa na huyo mwanamke....mwisho na yeye kuingia mitini.

Sasa nini kifanyike?, me naona ni bora sisi wanaume, tukajitaidi tukawachukulia hao single mother(s) katika hayo hayo madhaifu yao, hasa pale tunapokuwa tunawaitaji kimahusiano ya kimapenzi. Na ukiona unashindwa kufanya hivyo......basi ni mara mia ukazuia tamaa zako za kimwili, kwa lugha nyingine usitamani kuishi nao kimapenzi au jaribu kukaa nao mbali kabisa, maana kwa kushindwa kufanya hivyo, utakuwa unazidi kuiteketeza jamii yako kwa mna moja ama nyingine.

Na ikumbukwe kwamba, hao tunaowaita single mothers, wapo waliofanya uzembe kama vile kuzaa na mwanaume asiyemjua, kushindwa kulinda ndoa yake au kuzaa na mwanaume wa mtu....na mwisho kushindwa kuishi na huyo mwanaume, ilihali ameshazalishwa. Ila pia lipo kundi la pili, hili ni lile la single mothers, ambao walifiwa na waume zao, hivyo kujikuta wakibaki wenyewe wakilea watoto wao. Ni wazi utaona jinsi gani, kundi hili la pili, hao single mothers awaja visababishi vya moja kwa moja vya wao kuwapoteza waume zao....kama tunavyojua suala zima la kifo alina hodi. Ila pia kwa upande wa kundi la single mothers la kwanza, tunaona ni wazi walijisababishia matatizo, lakini usichukulie hiyo ndio ticket ya kuwadharau au kuwanyanyapaa kwa namna moja ama nyingine. Tukumbuke kwamba hao wote wanaweza kuwa mama zetu, Dada zetu, wake zetu, shangazi zetu au wanaweza kuwa hata bibi zetu pia.

Mwisho wa yote, naomba nitoe rahi kwa single mothers wote.....kwamba kuwa single mothers sio dhambi wala kosa kisheria. Hivyo mnatakiwa muondoe nafsi zote za majuto na kujihisi kutokuweza (kukaa tamaa), kisha muingie fields kiukakamavu na kujitafutia ridhiki kama kawaida ili muweze kulea watoto wenu vyema kabisa. Pili, naomba mjitaidi sana, na wala msijisikie aibu kuwaelekeza wadogo zenu au watoto wenu na jamii kwa ujumla....juu ya mema na mabaya mliyojifunza, ili kuisaidia jamii inayowazunguka. Na mwisho kabisa, naomba muwe makini sana, hasa pale linapokuja suala la kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa mara nyingine tena......ukiona unaweza kujizuia, its better ukajizuia kwani huko utaenda kujiongezea matatizo tu.

Asante.
 
Kwani singo maza hawezi kuwa alitoa mimba kabla? Anaweza kuwa kazaa na ashatoa mimba kadhaaa na mwinginw anaweza kuwa hajazaa na hajatoa mimba.
 
Truth to be told
Nawakubali sana single maza
 
Instagram inaharibu wadada aisee. Usiombe uwe na surbodinate single mother. Yaani she would literally make you feel guilty kama wewe ndio baba wa mtoto. All excuses asifanye kazi, as if it is a favor kwako kuwa she is a single mother and she is still working.

Khaaa!
Afadhali mnatokea mara moja moja kuwapa somo wadogo zenu.
 
Hao ni wavulana wasikuumize kichwa, wanaume wanajielewa.
 
Mkishatelekezwa na kurudi kutafuta huruma kwa mwamvuli wa usingo maza, ndo utajua definition ya Mme wa mtu...kwa sasa maana yake ndo hiyo mwanaume ni mwanaume
Hiyo comment imedhihirisha single maza wanajidharau kabla ya kudharauliwa, mtu kama huyo sio wakuoa ni wakuzalishwa!!




Samahani kama nitakuwa nimetumia maneno makali
 
Hiyo comment imedhihirisha single maza wanajidharau kabla ya kudharauliwa, mtu kama huyo sio wakuoa ni wakuzalishwa!!




Samahani kama nitakuwa nimetumia maneno makali
Mi huwa sielewi kabisa kwa hili special group lililojiibua siku hizi "singo maza" kuna siku nliona hadi kuna kipindi kabisa cha TV eti cha singo mazas serious???
Teh sijui nitaambiwa najishaua!!! Ila mie siwaelewi hii huruma wanohitaji kwa jamii ni ipi hasa
 
Afadhali umewapa ukweli.
 
Wanataka public sympath tena ya kipuuzi na yakupuuzwa! Sikatai singo mazas pia ni wanawake wengi wao wanatabia mbovu ndio maana ndoa zao zimevunjika wanabaki kutafuta huruma ya lazima... Tena kuna mmoja umemquote hapo kajidharau sanaaa!!
 
Wanataka public sympath tena ya kipuuzi na yakupuuzwa! Sikatai singo mazas pia ni wanawake wengi wao wanatabia mbovu ndio maana ndoa zao zimevunjika wanabaki kutafuta huruma ya lazima... Tena kuna mmoja umemquote hapo kajidharau sanaaa!!
Binafsi singo mama nnaowaonea huruma na kuelewa magumu yao ni waliofiwa, na walioteswa wakaona waendelee maisha yao. Hawa wanaojidanganya kuzaa na mwanaume mwenye ndoa yake wakidhani watapata free ride, wanaoona hawahitajiki ila wabajibebesha mimba kwa kudhani ndio njia ya kuwin moyo wa mtu, wanaokimbilia kuzibeba kama njia ya kuolewa WAPAMBANE NA HALI ZAO
 
Mimi bado sijafikilia swala la kuoa ila nakazana nao sana yaani akikupa anakupa hakubanii labda ushindwe wewe hiyo nawapa sifa yenu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…